Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Changamoto za uchaguzi wa wabunge na wa madiwani wa mikoa nchini Togo

Raia wa Togo watachagua wabunge wao na kwa mara ya kwanza madiwani waokatika mikoa siku ya Jumatatu, Aprili 29, chini ya mvutano mkubwa tangu kupitisha kwa Katiba mpya iliyopignwa ambayo itabadilisha nchi hiyo kuwa ya utawala wa bunge.

Raia wa Togo watapiga kura Jumatatu kuwachagua wabunge 113, ikilinganishwa na 91 mwaka wa 2018. Uhaguzi wa madiwani wa mikoa utakuwa wa kwanza katika nchi hii kugawanywa katika mikoa mitano.
Raia wa Togo watapiga kura Jumatatu kuwachagua wabunge 113, ikilinganishwa na 91 mwaka wa 2018. Uhaguzi wa madiwani wa mikoa utakuwa wa kwanza katika nchi hii kugawanywa katika mikoa mitano. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya baba yake, ambaye alitawala Togo kwa mkono wa chuma kwa karibu miaka 40, Rais Faure Gnassingbé, yeye mwenyewe madarakani tangu mwaka 2005, anashutumiwa na upinzani kwa kutaka kusalia madarakani kutokana na marekebisho ya katiba.

Nchini Togo, wabunge wanachaguliwa kwa muhula wa miaka mitano. Uchaguzi uliopita wa wabunge ulifanyika mwaka 2018 na rais wa Togo alihakikisha mwishoni mwa mwaka 2022 kwamba utafanyika mwaka 2023, kabla ya kuahirisha kalenda ya uchaguzi mara kadhaa.

Raia wa Togo watapiga kura siku ya Jumatatu kuwachagua wabunge 113, ikilinganishwa na 91 mwaka wa 2018. Chaguzi za madiwani wa mikoa zitakuwa za kwanza katika nchi hii kugawanywa katika mikoa mitano. Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, matokeo ya muda katika ngazi ya kitaifa yatatangazwa na Tume ya Uchaguzi "katika muda wa siku sita baada ya uchaguzi".

Uchaguzi wa serikali katika mikoa utachagua madiwani 179 wa mikoa ambao, pamoja na madiwani wa manispaa, watawachagua maseneta. Bunge la Seneti lilianzishwa kwa marekebisho ya katiba ya mwaka 2002 lakini halikuwekwa kamwe, na kwa hivyo uchaguzi wa madiwani utafanya iwezekane kuliweka.

"Kuanzia sasa na kuendelea, miswada na sheria zinazopendekezwa kwanza zitapelekwa mbele ya maseneta, ambao watalazimika kutoa maoni yao, kabla ya kupitishwa na wabunge," Pascal Agbové, mtaalamu wa masuala ya siasa, ameliambia shirika la habari la AFP.

Je, hali ya kisiasa ya sasa ikoje?

Imekuwa ya wasiwasi sana tangu kupitishwa Machi 25 katika hatua ya kwanza kwa Katiba mpya inayohamisha nchi kutoka kwa utawala wa rais hadi utawala wa bunge. Kupitishwa huku kwa katiba mpya kulisababisha ukosoaji mkubwa katika safu ya upinzani na mashirika ya kiraia, lakini Rais Gnassingbé aliomba uchunguzi upya wa maandishi, uliopitishwa kwa hakika mnamo Aprili 19 na wabunge.

Lakini upinzani unasalia kuwa na nguvu dhidi ya mageuzi haya na unashutumu "mapinduzi ya kitaasisi" yaliyopangwa kulingana upinzani huo kumruhusu Faure Gnassingbé kubaki madarakani.

Upinzani uko wapi?

Wakati wa chaguzi hizi zijazo, upinzani unajitayarisha kupinga chama tawala, Union for the Republic (UNIR), ingawa ulisusia uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2018 kwa kushutumu "makosa" katika sensa ya uchaguzi.

Uliwahamasisha sana wafuasi wake wakati wa sensa. Wapigakura milioni 4.2 wamesajiliwa kwenye orodha ya wapiga kura, au karibu nusu ya wakazi milioni 8.8 nchini humo, ikilinganishwa na milioni 3.1 waliosajiliwa mwaka wa 2018. Upinzani pia ulipinga daftari la uchaguzi mnamo mwezi wa Novemba lililooidhinishwa na jumuiya ya nchi zinazo zungumza Kifaransa (OIF), na unahofia "udanganyifu wa uchaguzi" wakati wa chaguzi hizi za ubunge.

Je, kupishana madarakani kunawezekana?

Rais Faure Gnassingbé amekuwa madarakani tangu 2005, akimrithi babake ambaye alishikilia hatamu ya nchi kwa karibu miaka 38.

"Hatupaswi kutarajia mengi kutoka kwa uchaguzi wa wabunge," Jean Yaovi Dégli, mwanasheria na waziri wa zamani anayehusika na uhusiano na Bunge (1991-1992) ameliambia shirika la habari la AFP. "Upinzani hauna uungwaji mkono wa kutosha chinichini ili kutafsiri kutoridhika kunakowezekana kwenye sanduku la kura," anaamini, bila kuondoa "mshangao", lakini "uchaguzi bado unahitaji kuwa wa uwazi na wa kidemokrasia.

Chini ya masharti ya Katiba mpya, ni wabunge na maseneta, waliokusanyika katika Congress, na si watu tena, ambao watamchagua Rais wa Jamhuri. Madaraka yatakuwa mikononi mwa Rais wa Baraza la Mawaziri. Kiongozi wa chama kilicho wengi katika Bunge la taifa atashika nafasi hii moja kwa moja. Kwa sasa, Faure Gnassingbé ndiye rais wa chama cha walio wengi, UNIR.

"Katika mfumo wa bunge, hakuna ukomo wa mamlaka, anayesimamia ni mwakilishi wa chama kilicho wengi katika Bunge. Ikiwa chama kinachoongoza hakina wingi wa viti, basi kutakuwa na kupishanamadarakani", anafafanua Jean Yaovi Dégli. .

"Chaguzi hizi sio za haki kwa sababu chama tawala kinatumia rasilimali za serikali, na kufanya kampeni, kunahitaji pesa," Michel Goeh-Akue, mwanahistoria aliye na uhusiano wa karibu na upinzani, ameliambia shirika la habari la AFP, ambaye anaona nchi ikiingia kwenye mzozo wa kupishana madarakani au mapinduzi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.