Pata taarifa kuu
KATIBA-USALAMA

Togo: Wabunge wapitisha Katiba mpya bila kizuizi chochote

Rasimu, iliyopigiwa kura mnamo Machi 25, imepitishwa kwa hatu ya pili siku ya Ijumaa Aprili 19 kwa ombi la Rais wa Jamhuri, Faure Gnassingbe. Baada ya marekebisho ya vifungu vichache, muswada ambao unabadilisha utawala wa Togo, na kuupeleka kwenye utawala wa bunge, umepitishwa kwa kura 87.

Makao makuu ya Bunge la taifa la Togo, Januari 8, 2019 mjini Lomé.
Makao makuu ya Bunge la taifa la Togo, Januari 8, 2019 mjini Lomé. © Wikimedia Commons CC0 Kayi Lawson (VOA)
Matangazo ya kibiashara

Muswada umepitishwa kwa kura 87 bila kupingwa. mara tu utakapotangazwa, Togo inahamia Jamhuri ya tano.

Muswada uliyopitishwa hau ya kwanza kwa kura 89 kati ya 91 haujachapishwa kwa ukamilifu. Lakini ilifuta uchaguzi wa moja kwa moja wa rais. Katika toleo hili, Rais wa Jamhuri, aliyechaguliwa bila mjadala na Bunge, alikuwa na jukumu la ishara. Madaraka yalishikiliwa na rais wa Baraza la Mawaziri, aliyechaguliwa kutoka chama cha walio wengi. Tangu wakati huo, muswada ulirejeshwa kwa kamati ya sheria, bado hatujui ni vifungu gani vimerekebishwa.

Ni Rais Faure Gnassingbé aliyeirudisha kwenye Bunge kwa ajili ya kupigiwa kura kwa mara ya pili, baada ya wimbi la ukosoaji. Baadhi ya vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia vinamshuku kiongozi huyo wa nchi, aliyekaa madarakani kwa miaka 19, kutaka kusalia madarakani kama mkuu wa nchi. Pia wanashutumu kura kwa maandishi ya kimsingi na wabunge ambao muda wao wa kazi umeisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.