Togo: Ecowas kujaribu kupata suluhu ya kisiasa baada ya mabadiliko ya katiba
Ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi kutoka nchi za Afrika Magharibi ECOWAS umekwenda nchini Togo, kujaribu kupata suluhu ya kisiasa kufuatia mabadiliko ya katiba yaliyozua hali ya sintofahamu kati ya wanasiasa.
Imechapishwa:
Cheza - 00:50
ECOWAS imesema imetuma ujumbe wake, kufanya mashauriano na wadau wote, wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kushiriki kwenye uchaguzi wa wabunge tarehe 29 mwezi huu.
Ujumbe huo unaongozwa na aliyekuwa mjumbe wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Mali na ukanda wa Sahel Maman Sambo Sidikou, ambaye anatarajiwa kutamatisha ziara yake siku ya Jumamosi.
Hali ya sintofahamu ya kisiasa inaendelea baada ya mwezi uliopita, wabunge kupitisha mabadiliko ya katiba kubadilisha mfumo wa uongozni nchini humo ambapo rais atachaguliwa na wabunge na sio wananchi, kwa muhula wa miaka sita.
Soma piaTogo yahirisha uchaguzi wa wabunge hadi Aprili 29
Wanasiasa wa upinzani, viongozi wa dini na mashirika ya kiraia, wanasema huu ni mpango wa rais Faure Gnassingbe, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2005 kuendelea kusalia madarakani.
Hillary Ingati- RFI-Kiswahili.