Pata taarifa kuu

Niger yatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku 3 baada ya shambulio lililoua watu 23

Maombolezo ya kitaifa ya siku 3 nchini Niger yametangazwa kuanzia leo baada ya shambulio lililosababisha vifo vya watu 23 katika safu ya jeshi usiku wa Jumatano Machi 20 kuamkia Alhamisi Machi 21, 2024, kulingana na ripoti kutoka kwa wizara ya ulinzi. 

Mohamed Toumba, mmoja wa wanajeshi waliompindua Rais wa Niger Mohamed Bazoum, akizungumza na wafuasi wa utawala wa kijeshi mjini Niamey, Niger, Jumapili Agosti 6, 2023.
Mohamed Toumba, mmoja wa wanajeshi waliompindua Rais wa Niger Mohamed Bazoum, akizungumza na wafuasi wa utawala wa kijeshi mjini Niamey, Niger, Jumapili Agosti 6, 2023. © Sam Mednick / AP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa operesheni ya jeshi kati ya maeneo ya Teguey na Bankilaré, katika jimbo la Tillabéri, jeshi lilivamiwa na zaidi ya magaidi mia moja waliokuwa kwenye magari na pikipiki, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Shambulio hilo lilitokea katika eneo la Tillabéri, linalojulikana kuwa maficho ya wanajihadi wa Sahel, wakiwemo wale wa Islamic State katika Greater Sahara na Al-Qaeda.

Wanajeshi 23 waliuawa katika "shambulio la kuvizia" lililotekelezwa na "magaidi" wakati wa "operesheni ya jeshi magharibi mwa Niger, wizara ya Ulinzi ya Niger ilitangaza siku ya Alhamisi usiku, Machi 21. Shambulio hilo lilitokea katika eneo la Tillabéri, lililoko katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu" kati ya Niger, Mali na Burkina Faso.

Eneo la Tillabéri ni maficho ya wanajihadi wa Sahel, wakiwemo wale wa EIGS na Al-Qaeda. Kwa miaka mingi, sehemu hii ya Niger imekuwa ikilengwa mara kwa mara na mashambulio ya makundi haya yenye silaha licha ya kutumwa kwa vikosi vya kupambana na wanajihadi.

Ramani inayoonyesha mji wa Tillabéri nchini Niger.
Ramani inayoonyesha mji wa Tillabéri nchini Niger. © RFI
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.