Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Togo kufanya uchaguzi wa wabunge Jumatatu

Hatimaye uchaguzi wa wabunge uliohirishwa nchini Togo, utafanyika siku ya Jumatatu, wakati huu nchi ikiwa kwenye sintofahamu ya kisiasa kufuatia mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Mabango ya uchaguzi ya chama cha UNIR kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge na mikoa nchini Togo, mjini Lome, Aprili 24, 2024.
Mabango ya uchaguzi ya chama cha UNIR kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge na mikoa nchini Togo, mjini Lome, Aprili 24, 2024. AFP - DODO ADOGLI
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika wakati huu, wapinzani wakisema rais Faure Gnassingbe anatarajiwa kutumia uchaguzi huo kuendeleza uongozi wake baada ya kuwa madarakani kwa miaka 20.

Wiki iliyopita, wabunge nchini Togo waliidhinisha mabadiliko ya katiba kubadilisha mfumo wa uongozi wa nchi hiyo kutoka ule wa urais hadi ule wa ubunge.

Rais atachaguliwa na wabunge na kuhudumu kwa muhula mmoja wa miaka minne, lakini mamlaka ya nchi hiyo, itakuwa chini ya Baraza la Mawaziri chini ya kiongozi wa chama kitakachokuwa na wabunge wengi bungeni.

Iwapo chama tawala cha rais Gnassingbe cha UNIR kitashinda uchaguzi wa wabunge, kuna uwezekano mkubwa kuwa atashika nafasi hiyo mpya kwa mujibu wa mabadiliko ya katiba.

Vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi wa mwaka 2018 kwa madai ya wizi wa kura, lakini wametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka huu ili kukiondoa chama cha UNIR madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.