Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Niger: Wanajeshi 23 wauawa katika shambulio la kuvizia lililotekelezwa na 'magaidi'

Shambulio hilo lilitokea katika eneo la Tillabéri, linalojulikana kuwa maficho ya wanajihadi wa Sahel, wakiwemo wale wa Islamic State katika Greater Sahara na Al-Qaeda.

Wanajeshi wa Niger wakipiga doria katika eneo lililo karibu na Bosso, katika jimbo la Diffa, Mei 25, 2015.
Wanajeshi wa Niger wakipiga doria katika eneo lililo karibu na Bosso, katika jimbo la Diffa, Mei 25, 2015. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi 23 waliuawa katika "shambulio la kuvizia" lililotekelezwa na "magaidi" wakati wa "operesheni ya jeshi magharibi mwa Niger, wizara ya Ulinzi ya Niger ilitangaza siku ya Alhamisi usiku, Machi 21. Shambulio hilo lilitokea katika eneo la Tillabéri, lililoko katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu" kati ya Niger, Mali na Burkina Faso.

Eneo la Tillabéri ni maficho ya wanajihadi wa Sahel, wakiwemo wale wa EIGS na Al-Qaeda. Kwa miaka mingi, sehemu hii ya Niger imekuwa ikilengwa mara kwa mara na mashambulio ya makundi haya yenye silaha licha ya kutumwa kwa vikosi vya kupambana na wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.