Pata taarifa kuu

Nigeria: Mamia ya wafungwa watoroka jela kutokana na mvua kubwa iliyonyesha

Takriban wafungwa 120 wametoroka kutoka jela nchini Nigeria baada ya mvua kubwa kuharibu ua wa jela hilo, mamlaka imesema siku ya Alhamisi.

Sehemu wanakofungwa wanawake katika moja ya jela nchini Nigeria.
Sehemu wanakofungwa wanawake katika moja ya jela nchini Nigeria. DR
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa iliyonyesha kwa saa nyingi siku ya Jumatano "iliharibu" kizuizi katika mji wa Suleja, katikati mwa Nigeria, karibu na mji mkuu Abuja, na kuharibu majengo na uzio wa ulinzi, amesema msemaji wa mmlaka ya magereza ya Nigeria. Uharibifu huu ulisababisha "kutoroka kwa jumla ya wafungwa 119 kutoka kwa jela hilo," ameongeza Adamu Duza, aliyenukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wafanyakazi wa magereza na maafisa wengine wa usalama waliweza kuwapata wafungwa 10, huku wengine wote wakiendelea kutafutwa, amesema. Bw Duza amekiri uchakavu wa magereza ya "zama za ukoloni" nchini Nigeria ambayo "ni kongwe na dhaifu", na akasema wakuu wa magereza wanafanya kazi kubadilisha "vituo vyote vya kuzeeka" kwa "vituo vya kisasa".

Mamlaka ya magereza imetoa wito kwa wananchi kuwa makini na wafungwa wanaotorok na kutoa taarifa kwa maafisa wa usalama. Kutoroka ni jambo la kawaida katika magereza yenye msongamano mkubwa wa watu nchini Nigeria, ambapo magenge ya wahalifu na wanajihadi hufanikiwa kuingia ili kuwaachilia wenzao.

Mnamo mwezi wa Julai 2022, wanajihadi waliingia kwenye gereza la Kuje nje kidogo ya mji wa Abuja wakiwa na vilipuzi na silaha nzito, na kuwaachilia wafungwa zaidi ya 800, wakiwemo wenzao zaidi ya 60.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.