Pata taarifa kuu

Wanajeshi sita wameuwa katika shambulio la watu wenye silaha nchini Nigeria

Wanajeshi sita wameripotiwa kuuawa katika shambulio la kuvizia katikati mwa Nigeria eneo ambapo maofisa wa jeshi wanakabiliana na makundi ya kihalifu, jeshi limethibitisha.

Maofisa wa jeshi nchini Nigeria wamekuwa wakikabiliana na wezi wa mifugo katikati mwa taifa hilo.
Maofisa wa jeshi nchini Nigeria wamekuwa wakikabiliana na wezi wa mifugo katikati mwa taifa hilo. AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Maeneo ya Kaskazini Magharibi na katikati mwa Nigeria kwa miaka sasa yamekuwa yakitatizwa na makundi ya watu wenye silaha wanaoshambulia vijiji na kuwateka raia, kuteketeza moto makazi ya watu na kisha kuiitisha kikombozi ilikuwaachia waliotekewa.

Makundi yao ya watu wenye silaha yamekuwa yakihusishwa na kuwa na ushirikiano na wanajihadi wanaoendeleza harakati zao katika eneo la kaskazini mashariki mwa taifa hilo kwa muda wa miaka 15 sasa.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, maofisa wake waliokuwa kazini siku ya Ijumaa katika eneo la Shiroro katika jimbo la Niger walishambuliwa na watu wenye silaha hatua ambayo iliwalazimu kujibu.

Wilaya ya Shiroro imetajwa kuwa makao ya mkuu wa wezi wa mifugo kwa jina la Dogo Gide, ambaye ameingia katika ushirikiano na kundi la Islamic State-linahusishwa na wanajihadi.

Mwezi Agosti, wapiganaji watiifu kwa Gide waliwaua wanajeshi 23 na raia watatu katika shambulio dhidi ya msafara wa walinda usalama katika jimbo la Niger.

Ndege ya kijeshi iliotumwa kuwanusuru majeruhi ilianguka na kusababisha vifo vya watu waliokuwa ndani yake, wezi wa mifugo wakidai kuwa walihusika na kuiangusha.

RFI-Kiswahili/ AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.