Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Matangazo ya BBC na Sauti ya Amerika yasitishwa kwa wiki mbili

Vyombo vya habari vya Uingereza na Marekani, BBC na Sauti ya Amerika (VOA), vimesitishwa kupeperusha matangazo kwa wiki mbili nchini Burkina Faso kwa kutangaza ripoti ya Human Rights Watch (HRW) inayolishutumu jeshi kwa "unyanyasaji" dhidi ya raia, mamlaka ya mawasiliano nchini Burkina Faso ilitangaza April 25, 2024.

Sehemu ya mbele ya Baraza Kuu la Mawasiliano huko Ouagadougou, Burkina Faso, Mei 2015.
Sehemu ya mbele ya Baraza Kuu la Mawasiliano huko Ouagadougou, Burkina Faso, Mei 2015. AFP - AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

 

Baraza Kuu la Mawasiliano (CSC) "limeamua kusimamisha vipindi vya vituo viwili vya redio vya kimataifa (BBC na VOA) vinavyorusha matangazo yao kutoka mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, kwa muda wa wiki mbili," inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka CSC. 

Mamlaka hiyo inahalalisha uamuzi huu na matangazo ya vyombo hivi vya habari viwili "kwa makala inayoshutumu jeshi la Burkina Faso kwa unyanyasaji dhidi ya raia".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.