Pata taarifa kuu

RSF: Sahel ni 'eneo kubwa zaidi lisilopata habari barani Afrika'

Kuangazia migogoro mingi katika Sahel kwa uhuru kunazidi kuwa vigumu kwa waandishi wa habari, hata zaidi tangu jeshi lichukue mamlaka katika baadhi ya nchi, shirika la Wanahabari Wasio na Mipaka "Reporters Without Borders" (RSF) katika ripoti iliyochapishwa leo Jumatatu.

RSF inalaani hatua za nchi ningi za Sahel kufunga baadhi ya vyombo  vya habari, magazeti ya kila siku na kuwafukuza waandishi wa habari.
RSF inalaani hatua za nchi ningi za Sahel kufunga baadhi ya vyombo vya habari, magazeti ya kila siku na kuwafukuza waandishi wa habari. AFP - ANNIE RISEMBERG
Matangazo ya kibiashara

Ukanda wa Sahel unaovuka bara kutoka magharibi hadi mashariki unatishia kuwa "eneo kubwa zaidi la Afrika lisilo na habari", inasema RSF katika ripoti hii mbaya. Kufukuzwa kwa waandishi wa habari wa Magazeti ya kila siku ya nchini Ufaransa, Le Monde na Liberation, hatua iliyochukuliwa na utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso siku ya Jumamosi imesabisha hali kuwa mbaya zaidi. Ripoti ya RSF iliandikwa kabla ya kufukuzwa kwao.

Vyombo vya habari vya ndani na kimataifa vimekuwa vikikabiliwa na "kuzorota mara kwa mara" kwa mazingira ya kazi kwa miaka kumi, inabaini ripoti hii inayohusu Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger, Chad, lakini pia kaskazini mwa Benin, nchi inayokabiliwa na changamoto kama hizo za usalama. Ripoti hii inaelezea waandishi wa habari walionaswa kati ya ghasia za wanajihadi na makundi yenye silaha kwa upande mmoja, na vikwazo, shinikizo, kusimamishwa kwa vyombo vya habari na kufukuzwa kwa waandishi wa habari wa kigeni na mamlaka kwa upande mwingine. Ripoti hiyo inaelezea hali mbaya iliyosababishwa na kuwasili kwa kampuni ya ulinzi ya kibinafsi ya Kirusi ya Wagner nchini Mali.

"Wanahabari watano waliuawa, na wengine sita walitoweka kati ya mwaka 2013 na 2023," ripoti hiyo inasema. Ripoti ya RSF inataja waandishi wa habari 120 waliokamatwa au kuzuiliwa katika kipindi hiki, wakiwemo 72 nchini Chad pekee. Pia inaripoti juu ya mashambulizi ya wanajihadi na kutoweka kwa redio za kijamii, ambazo zinasikilizwa na watu wengi, kwa sababu hazikuzingatia lengo lao.

Maeneo makubwa hayafikiki kwa waandishi wa habari kwa sababu ni hatari sana. Vyanzo "vinaogopa" kwa uwezekano wa kufanyiwa ukatili kutoka kwa makundi yyenye silaha, lakini pia kutoka kwa mamlaka. Nchini Mali, Burkina Faso na Chad, baada ya kufikia madaraka kwa shida, jeshi linataka "kudhibiti vyombo vya habari kwa njia za kupiga marufuku au vikwazo, hata mashambulizi au wanahabari kukamatwa kiholela".

RSF inakumbusha kusimamishwa kwa vyombo vya habari vya Ufaransa France 24 na Radio France Internationale nchini Mali na Burkina Faso. Kwa kufukuzwa au kulazimishwa kuondoka kwa waandishi wa habari wa kigeni kwa kukosa kibali, nafasi imepewa 'vyombo vya habari vinavyounga mkono Urusi au kutetea uwepo wa mamluki wa Wagner katika eneo hilo', hali ambayo inachangia 'kuwepo kwa habari potofu'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.