Pata taarifa kuu

Kenya: Kifo cha mwanahabari wa Pakistan Ashrad Sharif chaibua maswali

Baada ya kifo cha mwandishi wa habari maarufu wa Pakistani, aliyepigwa risasi na polisi takriban kilomita arobaini kutoka Nairobi siku ya Jumapili jioni, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International linataka uchunguzi huru ufanyike, huku magazeti kadhaa ya Kenya yakihoji toleo rasmi.

Mwandishi wa habari wa Pakistani Arshad Sharif akipiga picha mnamo Desemba 2016 kabla ya kipindi chake cha talk-show kwenye studio huko Islamabad.
Mwandishi wa habari wa Pakistani Arshad Sharif akipiga picha mnamo Desemba 2016 kabla ya kipindi chake cha talk-show kwenye studio huko Islamabad. AP
Matangazo ya kibiashara

"Je, ni makosa ya utambulisho au mauaji, ikifuatiwa na jaribio la kuficha? ". Swali lililoulizwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Standard Jumanne asubuhi. Katika safu zake, gazeti hilo la kila siku nchini Kenya linaorodhesha sehemu tatanishi za maelezo yaliyotolewa na polisi kufuatia kifo cha Ashrad Sharif.

Mwandishi huyo wa habari wa Pakistan aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi nchini Kenya, alikokuwa amekimbilia. Polisi wanarejelea "tukio la kusikitisha" na kusema gari lao lilidhaniwa kuwa gari lingine lililoripotiwa kuibwa ambapo ndani ya gari kulidaiwa kuwa na mtoto aliyetekwa nyara.

Mazingira ya mkasa huu "ni ya kutisha", limesema shirika la Amnesty International katika taarifa yake. Shirika hili linataka "uchunguzi huru" na linataja ripoti kadhaa kulingana na hali ambayo risasi nane hadi tisa zilifyatuliwa kwenye gari. 

Ni "mauaji ya kutatanisha", pia linashutumu shirika la Waandishi Wasio na Mipaka, RSF, ambalo pia linataka uchunguzi wa kimataifa kutoka Umoja wa Mataifa. "Hasa kwa vile mwanahabari huyu alitoroka nchi yake kwa kuhofia usalama wake, kunyanyaswa na kukamatwa," limeongeza Amnesty International.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.