Pata taarifa kuu

Mtangazaji maarufu wa televisheni wa Pakistani apigwa risasi na kufariki nchini Kenya

Mtangazaji nyota wa runinga wa Pakistan, ambaye alitoroka nchini humo miezi kadhaa iliyopita kwa kuhofia kukamatwa kwa uchochezi, amepigwa risasi na kuuawa nchini Kenya. Polisi inanyooshewa kidole kuhusika na mauaji hayo, kulingana na vyanzo rasmi.

Kulingana na ripoti ya polisi iliyoonwa na shirika la habari la AFP, gari lililokuwa limembeba Bw Sharif na mwanamume mwingine lilifyatuliwa risasi tisa Jumapili jioni lilipokuwa likipita kwenye kizuizi cha barabarani katika eneo la kijijini takriban kilomita 40 kutoka mji wa Nairobi.
Kulingana na ripoti ya polisi iliyoonwa na shirika la habari la AFP, gari lililokuwa limembeba Bw Sharif na mwanamume mwingine lilifyatuliwa risasi tisa Jumapili jioni lilipokuwa likipita kwenye kizuizi cha barabarani katika eneo la kijijini takriban kilomita 40 kutoka mji wa Nairobi. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Arshad Sharif alikuwa mkosoaji mkubwa wa jeshi la Pakistan na mfuasi wa Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan, ambaye aliondolewa madarakani mwezi Aprili kwa kura ya kutokuwa na imani naye.

"Raia wa Pakistani ameuawa kama inavyosemekana na polisi," Ann Makori, mkuu wa Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi nchini Kenya (Ipoa), amewaambia waandishi wa habari leo Jumatatu.

"Timu yetu ya majibu ya haraka tayari imetumwa kuchunguza kifo cha mwandishi huyo," ameongeza.

Kulingana na ripoti ya polisi iliyoonwa na shirika la habari la AFP, gari lililokuwa limembeba Bw Sharif na mwanamume mwingine lilifyatuliwa risasi tisa Jumapili jioni lilipokuwa likipita kwenye kizuizi cha barabarani katika eneo la kijijini takriban kilomita 40 kutoka mji wa Nairobi.

Ripoti hiyo haisemi ni nani aliyefyatua risasi hizo, lakini inaeleza kuwa gari hilo liliendelea na safari hadi lilipowasili katika nyumba ya raia mwingine wa Pakistan.

Hapo, Bwana Sharif alitangazwa kuwa alifariki, na "jeraha la risasi kichwani ambalo lilipenya kutoka nyuma".

Ripoti hiyo inaongeza kuwa wakati tukio hilo likifanyika, polisi ilikuwa ikitafuta gari lililokuwa limeibiwa pamoja na mtu ambaye alikuwa alitekwa. Lakini haelezi ikiwa tukio hilo lina uhusiano na kifo cha bwana Sharif.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.