Pata taarifa kuu

Kesi kuhusiana na mradi wa kujenga bomba la kusafirishia mafuta Uganda-Tanzania yaahirishwa

Kesi iliyowasilishwa Mahakamani jijini Paris na mashirika yasiyo ya kiserikali kupinga mradi wa  kampuni ya mafuta na gesi ya Ufaransa TotalEnergies, kujenga bomba la kusafirishia mafuta kutoka nchini Uganda kupitia nchini Tanzania, imeahirishwa mpaka Desemba tarehe 7 .

Licha ya kuendelea kwa kesi hii na wabunge wa Umoja wa Ulaya kupitisha azimio la kupinga mradi huo, rais wa Uganda Yoweri Museveni ameendelea kusisitiza kuwa mradi huu utaendelea kama ilivyopangwa.
Licha ya kuendelea kwa kesi hii na wabunge wa Umoja wa Ulaya kupitisha azimio la kupinga mradi huo, rais wa Uganda Yoweri Museveni ameendelea kusisitiza kuwa mradi huu utaendelea kama ilivyopangwa. REUTERS - STEPHANE MAHE
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya mawakili wa wanaharakati hao wanaopinga ujenzi wa bomba hilo kwa kile wanachosema utaharibu mazingira na kuhatarisha maisha ya binadamu, kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo, ili kupata muda wa kujibu utetezi wa kampuni ya Total. 

Hata ivyo, kabla ya pande mbili kuanza kutoa utetezi wao mwezi Disemba, kutakuwa na kikao maalum tarehe 26 mwezi Oktoba, ambako watalaam wa sheria watakutana kukubaliana kuhusu mwenendo wa kesi hiyo. 

Mwaka  2019, wanaharakati hao kutoka mashirika sita wakiwemo wale nchini Uganda walifika Mahakamani kuishataki kampuni hiyo kwa kukiuka sheria ya Ufaransa ya mwaka 2017 inayotaka ulinzi wa haki za binadamu na mazingira, na kutaka kampuni kusitisha mradi huo. 

Licha ya kuendelea kwa kesi hii na wabunge wa Umoja wa Ulaya kupitisha azimio la kupinga mradi huo, rais wa Uganda Yoweri Museveni ameendelea kusisitiza kuwa mradi huu utaendelea kama ilivyopangwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.