EU : Yafadhili Kenya kupambana na Ebola
Ujumbe wa umoja wa Ulaya nchini Kenya, umetoa dolla 98,224.59 , kwa taifa hilo ambapo zitatumika kuhamasisha umma dhidi ya ugonjwa wa Ebola, baada ya taifa jirani la Uganda kutangaza mkurupuko wa ugonjwa huo Septemba 20, mwaka huu, katika wilaya ya Mubende.
Imechapishwa:
Mchango huo wa EU, utatolewa kupitia kwa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, ambapo shirika hilo litaendesha uhamasisho mbali na kutoa elimu kwa wakaazi wa Kenya, wanaoishi karibu na miji ya mipani, ya namna ya kujikinga dhidi ya Ebola.
Mradi huu wa miezi tatu unalenga zaidi ya raia 565, 000, wenyeji wa miji ya mipakani ya Busia, Bungoma, Siaya, Kisumu, Homa Bay na Migori
Elimu hii inatolewa kutokana na taasubi ambazo zimekuwepo ikiwemo kwamba Ebola inasabishwa na ushirikina, elimu hii ikilenga viongozi wa dini, waganga wa kienyeji na raia wa kawaida.
Eerikali ya Kenya, kupitia wizara yake ya afya, tayari imetoa tahadhari kwa raia wake kujikinga dhidi ya Ebola.
Serikali ya Uganda imethibitisha vifo 25 kutokana na Ebola , na wagonjwa 61 hadi kufikia Oktoba 18.