Pata taarifa kuu

Mlipuko wa Ebola nchini Uganda: Vifo 29 vyaripotiwa, wakiwemo wahudumu wanne wa afya

Watu 29, wakiwemo wahudumu wanne wa afya, wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Uganda tangu mamlaka ilipotangaza mlipuko wa ugonjwa huo katikati mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita, Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema Jumatano.

Daktari anafanya kazi katika maabara ya kupima sampuli zilizokusanywa za virusi vya Ebola katika Kituo cha Kudhibiti Magonjwa huko Entebbe, yapata kilomita 37 (maili 23) kusini magharibi mwa mji mkuu wa Uganda Kampala, Agosti 2, 2012.
Daktari anafanya kazi katika maabara ya kupima sampuli zilizokusanywa za virusi vya Ebola katika Kituo cha Kudhibiti Magonjwa huko Entebbe, yapata kilomita 37 (maili 23) kusini magharibi mwa mji mkuu wa Uganda Kampala, Agosti 2, 2012. REUTERS/Edward Echwalu
Matangazo ya kibiashara

"Wagonjwa 63 waliothibitishwa na wametambuliwa, ikiwa ni pamoja na vifo 29," Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema katika mkutano wa waandishi wa habari. Ameeleza kuwa "wahudumu kumi wa afya wameambukizwa na wanne wamefariki".

Uganda imewahi kukumbwa na milipuko ya ugonjwa wa Ebola, ugonjwa ambao umegharimu maelfu ya maisha barani Afrika tangu ulipogunduliwa mwaka 1976 katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mamlaka ya afya ya nchi hii ya Afrika katika eneo la Maziwa Makuu ilitangaza mnamo Septemba 23 kifo cha mtu mwenye umri wa miaka 24 baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola katika eneo la kati la Mubende, ikiwa ni kifo cha kwanza tangu 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.