Pata taarifa kuu

Kifo cha mwandishi wa habari nchini Rwanda: RSF yashutumu utaratibu 'usio wazi'

Kesi za kisheria juu ya kifo cha mwandishi maarufu wa habari nchini Rwanda, mkosoaji wa utawala wa Rais Paul Kagame, "hazieleweki" na "kusababisha wengi kujiuliza maswali mengi", limelaani shirika la Wanahabari Wasio na Mipaka (RSF), likibaini kuwa aliuawa 'kimakusudi'.

John Williams Ntwali, 44, mhariri wa gazeti la The Chronicles, alifariki Januari 18 wakati gari lilipogonga pikipiki aliyokuwa amepanda akiwa abiria karibu na mji mkuu wa Kigali.
John Williams Ntwali, 44, mhariri wa gazeti la The Chronicles, alifariki Januari 18 wakati gari lilipogonga pikipiki aliyokuwa amepanda akiwa abiria karibu na mji mkuu wa Kigali. Β© Arquivo pessoal
Matangazo ya kibiashara

John Williams Ntwali, 44, mhariri wa gazeti la The Chronicles, alifariki Januari 18 wakati gari lilipogonga pikipiki aliyokuwa amepanda akiwa abiria karibu na mji mkuu wa Kigali.

Dereva aliyehusika katika ajali hiyo, ambaye alikiri makosa, alihukumiwa Februari 7 kulipa faini ya faranga milioni moja za Rwanda, takriban euro 860. RSF, ambayo inashtumu katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa ni "kesi isiyoeleweka", Β na "inashutumu utaratibu usio wazi ambao unaacha maeneo mengi kuhusiana na mazingira ya kifo chake".

"Hukumu hii ilitolewa kwa msingi wa uchunguzi ambao haujawahi kuwekwa wazi na ambao ni wazi ulizingatia dhana ya ajali, bila kuchunguza njia zingine", kulingana na RSF, na kuongeza: "Mwaka 2012, mwandishi wa habari, ambaye tayari alitishiwa, alikuwa mwathirika wa ajali kama hiyo ambayo alinusurika."

"Euro 860, hii ni bei ya mauaji ya mwandishi wa habari nchini Rwanda?" anauliza mkurugenzi wa ofisi ya RSF barani Afrika, Sadibou Marong, katika taarifa kwa vyombo vya habari. Katika ukurasa wake wa Twitter mnamo Januari 23, msemaji wa serikali Yolande Makolo alizungumzia 'tuhuma zisizo na msingi'.

Mwishoni mwa mwezi Januari, mashirika 90 ya haki za binadamu, hasa ya Kiafrika, yalitoa wito kwa mamlaka ya Rwanda kwa "uchunguzi huru, usiopendelea na wenye ufanisi" ambao ungetegemea "wataalam wa kimataifa", baada ya "kifo cha ghafla" cha mwandishi huyo wa habari maarufu.

"Ntwali", kama wengi walivyomwita, alifungwa gerezani mara nyingi wakati wa kazi yake, wakati mwingine kwa saa chache, wakati mwingine wiki kadhaa. Alianzisha chaneli ya Pax TV kwenye YouTube, hasa ikitangaza mahojiano, kwa Kinyarwanda, yenye sauti za wapinzani.

Tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ambayo yalisababisha vifo vya watu 800,000 hasa Watutsi, Rwanda imetawaliwa kwa mkono wa chuma na Paul Kagame. Akisifiwa kwa mafanikio ya sera yake ya maendeleo, rais huyo pia anakosolewa na mashirika ya haki za binadamu kwa ukandamizaji wake wa uhuru wa kujieleza.

Nchi hiyo iko katika nafasi ya 136 kati ya nchi 180 kwa uhuru wa vyombo vya habari RSF. "Tangu 1996, wataalamu wanane wameuawa au wametoweka, na 35 wamelazimishwa kwenda uhamishoni," linaandika shirika la RSF hususan kwenye tovuti yake. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, vyombo vya habari huru vilikuwa nadra, na kuzuiwa na serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.