Pata taarifa kuu

Burkina Faso yasitisha matangazo ya kituo cha Ufaransa cha LCI

Mamlaka ya udhibiti wa vyombo vya habari nchini Burkina Faso imeamua kufunga matangazo ya kituo cha habari cha Ufaransa cha LCI kwa muda wa miezi mitatu, baada ya matamshi ya mwandishi wa habari kuhusu hali inayohusishwa na ghasia za wanajihadi kutajwa kuwa "habari za uongo".

Nembo za France 24 na LCI.
Nembo za France 24 na LCI. Montage /RFI
Matangazo ya kibiashara

Programu za LCI "zimesimamishwa kwa muda wa miezi mitatu nchini Burkina Faso kwenye mashada ya msambazaji yeyote wa huduma za sauti, hatua ambayo imeanza kutekelezwa baada ya kutangazwa uamuzi huu", limebaini Baraza Kuu la Mawasiliano (CSC), katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi.

Kulingana na CSC, LCI, kituo cha kibinafsi ca kundi la TF1, "kilitangaza Aprili 25, 2023, kipindi kiitwacho '24h Pujadas, l'info en question', ambapo mwandishi wake wa habari, Abnousse Shalmani, alitoa habari kadha kuhusu mzozo wa usalama katika eneo lq Sahel kwa ujumla lakini pia nchini Burkina Faso".

CSC inamkosoa mwandishi wa habari hasa kwa kuthibitisha kwamba "'wanajihadi' wanasonga mbele kwa kasi kubwa bila kuwepo kwa serikali yoyote katika maeneo yaliyotekwa", kwa kubainisha, "bila kutaja chanzo, kwamba 40% ya eneo linakaliwa na 'wanajihadi'" au kwamba "karibu raia 90,000 wanaojitolea kusaidia vikosi vya usalama (VDP) wanatumiwa 'kama kafara' kulinda askari wa Burkina Faso dhidi ya magaidi".

Mamlaka ya udhibiti a vyombo vya habari inaona kuwa matamshi haya ni "makisio rahisi na uzushi", baadhi "huenda yakazua machafuko ndani ya watu na kudhoofisha ushirikiano unaohitajika kati ya jeshi na raia kwa ajili ya kulinda nchi ya Burkina Faso".

Mwanzoni mwa mwezi Aprili, mamlaka ya mpito nchini Burkina Faso, ambayo inaongozwa na Ibrahim Traoré aliyeingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwezi Septemba, iliwatimua waandishi wa Magazeti ya kila siku ya Ufaransa ya Liberation na Le Monde.

Mwishoni mwa mwezi Machi, iliagiza kusitishwa kwa matangazo ya televisheni ya France 24, baada ya kusimamishwa mnamo mwezi Desemba 2022 Radio France Internationale (RFI), vyombo vya habari vya umma vya Ufaransa. Hata hivyo serikali ilihakikisha kuendelea "kushikamana" na uhuru wa kujieleza na maoni.

Burkina imenaswa tangu mwaka 2015 katika msururu wa machafuko ya wanajihadi yaliyotokea nchini Mali na Niger miaka michache mapema na ambayo yameenea nje ya mipaka yao. Ghasia hizo zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 10,000, raia na wanajeshi, kwa miaka minane, kulingana namashirika yasiyo ya kiserikali, na zaidi ya wakimbizi wa ndani milioni mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.