Pata taarifa kuu

Niger: ECOWAS yaombwa kutoa shinikizo ili Bazoum aachiliwe, kabla ya mkutano wa kilele

Mawakili wa rais wa Niger Mohamed Bazoum aliyepinduliwa na wanajeshi Julai 26, na kushikiliwa mfungwa tangu wakati huo, wameiomba Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, siku ya Ijumaa kushinikiza mteja wao aweze kuachiliwa kwake, kwa kwa utekelezaji wa uamuzi wa mahakama, katika mkesha wa mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo ya Nchi za Afrika Magharibi.

Mnamo Desemba 15, Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) iliagiza kuachiliwa kwa rais Bazoum na kurejea madarakani.
Mnamo Desemba 15, Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) iliagiza kuachiliwa kwa rais Bazoum na kurejea madarakani. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Desemba 15, Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) iliagiza kuachiliwa kwa rais Bazoum na kurejea madarakani.

"Ni jukumu la ECOWAS na nchi wanachama wake kuhakikisha kwamba maamuzi ya mahakama yanatumika ipasavyo na kwamba rais Bazoum na mkewe wanaachiliwa huru," amesema Mohamed Seydou Diagne, mratibu wa jumuiya ya wanasheria, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP. "Mahakama iliagiza mamlaka ya kijeshi kuwaachilia mara moja na kurejesha mamlaka ya rais Bazoum, ambaye mamlaka yake ilikabidhiwa kwake kidemokrasia," linabainisha kundi la wanasheria katika nakala hii.

Kulingana nao, Mohamed Bazoum hajawahi kuwasilishwa kwa hakimu na hajapata kutembelewa - mbali na ile ya daktari wake - tangu Oktoba 19, 2023. Mwanzoni mwa Januari, mtoto wa Mohamed Bazoum, Salem, aliachiliwa na kuhamishwa mara moja. kwenda Togo ambako yuko kwa sasa. Bado anatuhumiwa kwa "njama zinazolenga kudhoofisha mamlaka au usalama wa Serikali".

Mnamo tarehe 13 Februari, mkuu wa utawala wa kijeshi wa Niger Abdourahamane Tiani alisema katika mahojiano kwenye televisheni ya taifa kwamba kuachiliwa kwa Bw. Bazoum "hakukuwa kwenye ajenda." Mkutano wa kilele usio kuwa wa kawaida wa ECOWAS umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi mjini Abuja, Nigeria, kuchunguza hali ya kisiasa na usalama katika eneo hilo.

Niger, inayotawaliwa na utawala wa kijeshi tangu Julai 26 na kuwekewa vikwazo vikali na ECOWAS tangu wakati huo, ilitangaza kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi mwezi uliopita. Majirani na washirika wake wawili, Burkina na Mali, pia chini ya udhibiti wa jeshi, pia wamechagua chaguo hili.

Tawala hizo tatu za kijeshi zinaendelea kulaani Ufaransa kuitumia ECOWAS. "Chini ya Ibara ya 91 ya Mkataba Uliofanyiwa Marekebisho wa ECOWAS", Niger inatakiwa kuendelea "kutekeleza wajibu wake" kwa muda wa mwaka mmoja, wamekumbusha mawakili wa Mohamed Bazoum, katika taarifa yao ya siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.