Pata taarifa kuu

Miezi mitatu baada ya mapinduzi, Niger yatumbukia katika mgogoro

Nchini Niger, itakuwa ni miezi mitatu Alhamisi hii tangu jeshi lilipompindua Rais Bazoum na kuchukua madaraka. 

Moja ya mitaa ya mji wa Niamey, Niger, tarehe 2 Agosti 2023.
Moja ya mitaa ya mji wa Niamey, Niger, tarehe 2 Agosti 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Julai 28, Jenerali Abdourahamane Tiani aliteuliwa na jeshi kuwa rais wa CNSP, Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa taifa. Lakini kwa haraka, sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa ililaani mapinduzi haya. Inaendelea kudai kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba, ambao jeshi limeendelea kufutilia mbali. Matokeo: nchi hiyo imekuwa chini ya vikwazo vya ECOWAS tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, huku Ulaya na Marekani zikikata misaada yao.

Siku 91 baada ya mapinduzi hayo, kadri Niger inavyozidi kutumbukia katika mgogoro, ndivyo utawala wa kijeshi unavyozidi kuchukuwa hatua dhidi ya wale wanaopinga mamlaka yake. Mnamo Alhamisi, Oktoba 19, utawala wa kijeshi ulimshutumu Mohamed Bazoum kwa kujaribu kutoroka, bila kutoa ushahidi thabiti. Viongozi kadhaa wa utawala wa zamani wanashikiliwa na jeshi, na vyama vya kisiasa vimesitishwa. Akishtumiwa hasa kwa ujasusi kwa usirikiano na nchi ya kigeni, mwandishi wa habari Samira Sabou alizuiliwa kwa siku 8 mwanzoni mwa Oktoba.

Hali inayoelezewa na kuzorota kwa hali ya uchumi. Utawala mpya  wa kijeshi ulilazimika kupunguza bajeti ya kitaifa kwa 40%, na hofu ya kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wa umma. Matokeo: miradi mingi imesitishwa, kama vile ujenzi wa bwawa la Kandadji. Nchi wakati huo huo inakabiliwa na matatizo ya usambazaji kutokana na vikwazo vilivyochukuliwa na ECOWAS.

"Uhaba wa bidhaa mbalimbali waripotiwa"

Kutokana na hali hii, utawala wa kijeshi unajaribu kuleta chakula kutoka Burkina Faso, bila shida. "Pamoja na kuzorota kwa hali ya usalama, inakuwa ngumu zaidi kusindikiza malori," anaeleza mwanauchumi Ibrahim Adamou Louche. Yote hii ina maana kwamba raia wanaanza kukabiliwa na hali ngumu, anaeleza. Bidhaa za ndani, watu wanaendelea kutumia, hazitadumu milele. Na tunahisi kuwa mambo yanaanza kuwa magumu. Uhaba huo unazidi kushika kasi katika familia nyingi. Hali inazidi kuwa ngumu na watu wanaanza kuhoji kuhusu siku zijazo. Kando na hili, mfumuko wa bei unaendelea kuongezeka.

Ili kujaribu kuzuia hali hii ya mzozo, jeshi linacheza zaidi kuliko hapo awali juu ya roho ya utaifa. Fuko la mshikamano kwa ajili ya kulinda nchi ilizinduliwa hivi majuzi. raia wametakiwa kuchangia kifedha kwa minajili ya kuendesha shughuli za serikali.

Katika muda wa wiki moja tu, kulingana na serikali kila siku, faranga za CFA milioni 150 zinakusanywa, au chini kidogo ya euro 230,000.

Kutokana na hali hii ya kutisha, utawala wa kijeshi unaanza kutoa wito kwa ECOWAS. Siku ya Jumapili, Jenerali Mohamed Boubacar Toumba, Waziri wa Mambo ya Ndani, hakuondoa wazo la kuanza tena majadiliano na Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi. "Tuko hapa kufanya mazungumzo," alibaini waziri huyo mbele ya mwandishi wetu Serge Daniel, "ingawa jambo hili linaweza kukushangaza, labda ni sisi ambao tunataka mazungumzo, sio ECOWAS tena ambayo imejiweka imara na kusisitiza kuwa inataka kushambulia Niger. Lakini kilicho hakika ni kwamba ahadi kama hiyo itakuwa hatari kwa ECOWAS. Badala yake, tunataka kuona mshikamano wao kwa kuja kupambana na ugaidi huu kwa sababu wasisahau kwamba Niger ni nchi mojawapo inayokumbwa na mashambulizi ya magaidi. Leo hii, kuleta machafuko nchini Niger pia kunamaanisha kuwapokea magaidi hawa kwenye mipaka yao. "

Je, ni kweli utawala wa kijeshi uko tayari kurudi kwenye meza ya mazungumzo? Ndiyo, anabaini mtafiti kutoka Côte d'Ivoire Arthur Banga. "Nadhani mawasiliano yamefanywa kupitia Togo na kupitia baadhi ya machifu wa kimila na Nigeria," anasema kabla ya kuongeza: "Utawala wa kijeshi unaweza kuanza tena mazungumzo na ECOWAS kwa sababu hata kama leo umejiondoa kidogo, bado unaendelea kuwa mhusika muhimu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.