Pata taarifa kuu

Niger: Jeshi 'kumfungulia mashtaka' Rais Mohamed Bazoum kwa 'uhaini mkubwa'

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa usiku wa Jumapili, Agosti 13, viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Niger wametangaza kwamba "wana ushahidi wa kumshtaki rais aliyeondolewa madarakani na washirika wake wa ndani na nje kwa uhaini mkubwa." na kuhatarisha usalama wa ndani na nje wa Niger”.

Rais wa Niger Mohamed Bazoum katika mkutano wa WAEMU mjini Bissau, Julai 8, 2023.
Rais wa Niger Mohamed Bazoum katika mkutano wa WAEMU mjini Bissau, Julai 8, 2023. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Niger Mohamed Bazoum ambaye aliondolewa madarakani na kuzuiliwa tangu Julai 26 baada ya mapinduzi yaliyoongozwa na wanajeshi, anakabiliwa na shutuma mpya kutoka kwa jeshi. Jeshi ambalo liliunda serikali katika kipindi hiki cha machafuko nchini Niger, limetangaza usiku wa Agosti 13 kwamba wana nia ya "kumshtaki" mkuu wa nchi aliyeondolewa mamlakani kwa 'uhaini mkubwa' na 'kuhatarisha usalama' wa nchi.

"Serikali ya Niger hadi sasa imekusanya" "ushahidi wa kumfungulia mashitaka rais aliyeondolewa madarakani na washirika wake wa ndani na nje kwa mamlaka ya kitaifa na kimataifa kwa uhaini mkubwa na kuhatarisha usalama wa ndani na nje wa Niger", ametangaza kanali Meja Amadou Abdramane, mmoja wa wajumbe wa serikali, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa. Msemaji huyo anabaini kwamba rais huyo anayezuiliwa alirekodiwa njia ya simu.

Mohamed Bazoum, familia yake na washirika wake kadhaa wa karibu bado wanazuiliwa katika chumba cha chini cha makazi ya rais huko Niamey. Siku ya Jumamosi Agosti 12, rais wa Niger alitembelewa na daktari wake wa kibinafsi. Kulingana na daktari huyo, wote wanaozuiliwa "wanaendelea vyema" na Mohamed Bazoum "naye iko vizuri kiafya". Lakini rais Bazoum alisema kuwa matibabu yaliyotengwa kwa ajili ya familia yake na yeye mwenyewe ni "ya kinyama na ya kikatili".

Siku ya Jumapili, mamlaka ya kijeshi pia ilishutumu vikwazo "haramu, vya kinyama na vya kufedhehesha" vya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo inapinga mapinduzi hayo na kutishia kuivamia nchi hiyo ili kurejesha utawala wa kikatiba, ingawa njia ya diplomasia inapendekezwa kila wakati.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.