Pata taarifa kuu

Niger: ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka Nigeria wapokelewa mjini Niamey

Baada ya ziara nchini Niger ya machifu wa kimila kutoka nchi jirani ya Nigeria, ambao walikutana na Jenerali Abdourahamane Tiani mapema wiki hii, nao viongozi wa kidini wa Nigeria wamewasili Niamey.

Ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka Nigeria umepokelewa katika uwanja wa ndege wa Diori Hamani na Waziri Mkuu mpya wa kiraia, Ali Mahaman Lamine Zeine.
Ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka Nigeria umepokelewa katika uwanja wa ndege wa Diori Hamani na Waziri Mkuu mpya wa kiraia, Ali Mahaman Lamine Zeine. AP - J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo umepokelewa katika uwanja wa ndege wa Diori Hamani na Waziri Mkuu mpya wa kiraia, Ali Mahaman Lamine Zeine.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Nigeria (ANP), ni ujumbe wa viongozi wa kidini wa dini ya Kiislamu. Chanzo hiki kinaongeza kuwa wajumbe "walikutana mapema wiki hii huko Abuja na rais wa sasa" wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), na pia rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ili kujaribu upatanishi kati ya ECOWAS na Niger. 

Usuluhishi huu unakuja wakati Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ikiendelea kupendelea utatuzi wa mgogoro huo kupitia njia za kidiplomasia. Lakini majaribio ya hapo awali ya upatanishi hayajazaa matunda. Siku ya Jumanne, utawala wa kijeshi ulikataa kupokea ujumbe wa pamoja kutoka ECOWAS, Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa. Kwa hivyo, jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi imefahamisha kuwa iko tayari kupeleka kikosi cha kuingilia kati ili kumrejesha Rais Bazoum katika majukumu yake.

Hali ya uingiliaji kati kijeshi haiungwi mkono na nchi zote katika kanda hii. Nchini Nigeria kwenyewe, wabunge na viongozi wa kisiasa wamepaza sauti hadi kwenye Bunge la Seneti, wakimwomba rais Bola Tinubu kufikiria upya uwezekano wa ECOWAS kuingilia kijeshi nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.