Pata taarifa kuu

Je, Jumuiya ya ECOWAS inaundwa na nchi zipi na majukumu yake ni nini ?

Nairobi – ECOWAS au CEDAO, ni jumuiya ya Kiuchumi inayoundwa na mataifa 15 kutoka ukanda wa Afrika Magharibi, na makao yake makuu ni Abuja nchini Nigeria. 

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ndiye mwenyekiti wa ECOWAS
Rais wa Nigeria Bola Tinubu ndiye mwenyekiti wa ECOWAS © Ben Curtis / AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa, wanachama wanne wa jumuiya hiyo wamesimamishwa wanachama baada ya jeshi kuchukua madaraka kwa nguvu. Nchi zilizowasilishwa ni pamoja na Burkina Faso, Guinea, Mali na sasa Niger. 

Rais wa sasa wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu ndiye kiongozi wa jumuiya hiyo. Anaongoza kikao cha marais wa nchi wanachama kichofanya maamuzi ya kisiasa na kiuchumi yanayoathiri Jumuiya hiyo. 

Jumuiya hiyo pia inashirikiana kwenye masuala ya kijeshi kwa mujibu wa mkataba uliotiwa saini 2004, ina kikosi cha wanajeshi 6500 ambacho kimewahi kutumika katika operesheni za kulinda amani na kuresha utulivu wa kisiasa katika mataifa ya Guinea Bissau, Ivory Coast, Sierre Leone na Gambia. 

Jumuiya ya ECOWAS haina tofauti na ile ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambayo pia inahimiza utengamano wa watu na kushirikisha wananchi wa mataifa hayo saba kwenye shughuli za kiuchumi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.