Pata taarifa kuu

ECOWAS yaendelea na mazungumzo licha ya ujumbe wake kukataliwa kupokelewa Niger

Katika taarifa fupi kwa vyombo vya habari, ECOWAS inasema imepokea hatua ya viongozi wa mapinduzi nchini Niger kukataa kupokea wajumbe wa Umoja wa Afrika, ECOWAS na Umoja wa Mataifa. Ili kuhakikisha kurejea kwa utaratibu wa kikatiba, ECOWAS inasema itaendelea "kupeleka hatua zote muhimu", inaongeza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu (akivalia nguo ya bluu), ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS, akiwa amezungukwa na wenzake, wanachama wa jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi, Julai 30, 2023, kwa ajili ya mkutano maalum wa kilele uliohusu mapinduzi ya kijeshi nchini Niger.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu (akivalia nguo ya bluu), ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS, akiwa amezungukwa na wenzake, wanachama wa jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi, Julai 30, 2023, kwa ajili ya mkutano maalum wa kilele uliohusu mapinduzi ya kijeshi nchini Niger. AP - Chinedu Asadu
Matangazo ya kibiashara

Saa 24 kabla ya mkutano mwingine wa wakuu wa nchi za ECOWAS kuhusu Niger, uliopangwa kufanyika Alhamisi Agosti 10 huko Abuja, baadhi ya viongozi wa kanda hiyo hawafichi kutoridhika kwao, anaripoti mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Kwa mujibu wa taarifa kutokaRFI, ECOWAS iliwaalika maafisa kigeni kwenye mkutano wake wa kilele siku ya Alhamisi, akiwemo Emanuela Del Re, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya katika kanda ya Sahel.

Wakati ECOWAS ilikuwa imekaa kimya tangu kumalizika kwa makataa yake Jumapili jioni, rais wa Nigeria na Mwenyekiti wa ECOWAS, Bola Tinubu, amesisitiza kwamba diplomasia inasalia kuwa "njia bora" katika kukabiliana na mgogoro huo, hata kama bado hajaweka kando hatua ya kuingilia kati kijeshi.

Yeye na viongozi wa nchi nyingine za ECOWAS "wanapendelea azimio lililofikiwa kwa njia za kidiplomasia, kwa njia za amani, badala ya nyingine yoyote", ameongeza msemaji wa Bola Tinubu, Ajuri Ngelale, akibainisha kuwa msimamo huu utadumishwa, kwa kusubiri azimio lingine ambalo linaweza kucukuliwa au la katika mkutano usio kuwa wa kawaida wa ECOWAS uliopangwa kufanyika Alhamisi." "Tunatarajia maamuzi muhimu kuchukuliwa" katika mkutano huu, amebainisha msemaji wa rais Bola Tinubu, bila kutoa maelezo zaidi.

"Hakuna chaguo ambalo limekataliwa na ECOWAS", hata hivyo, alibainisha msemaji huyo. "Kila maisha ya binadamu ni muhimu, na hiyo ina maana kwamba kila uamuzi utakaochukuliwa na kambi ya (Afrika Magharibi) utajikita kwa kuzingatia amani, utulivu na maendeleo, sio tu ya kanda hiyo, bali pia ya bara la Afrika," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.