Pata taarifa kuu

Uongozi wa Kijeshi nchini Niger waeleza kutokutana na ujumbe wa ECOWAS

Uongozi wa kijeshi nchini Niger, umesema hauwezi kukutana na ujumbe kutoka Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, kwa sababu za kiusalama.

Mwenyekiti wa Ecowas ambaye pia ni rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, alipokuwa akihutubia marais kutoka nchi za ECOWAS mjini Abuja mnamo Julai 30, 2023. (Photo by Kola SULAIMON / AFP)
Mwenyekiti wa Ecowas ambaye pia ni rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, alipokuwa akihutubia marais kutoka nchi za ECOWAS mjini Abuja mnamo Julai 30, 2023. (Photo by Kola SULAIMON / AFP) AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Kupitia kwa barua iliyowasilishwa kwa mwakilishi wa ECOWAS jijini Niamey, uongozi huo wa kijeshi umesema mazingira kwa sasa sio rafiki kwa wao kukutana na ujumbe wa ECOWAS kwa sababu ya hasira ya wananchi baada ya Jumuiya hiyo kuiwekea vikwazo nchi yao.

Wiki iliyopita, ujumbe wa ECOWAS ulikwenda jijini Niamey kukutana na uongozi huo wa kijeshi lakini haukufanikiwa.

Jeshi nchini Niger, limetoa maelezo hayo wakati huu wakuu wa nchi za ECOWAS wakitarajiwa kukutana jijini Abuja nchini Nigeria siku ya Alhamisi, kuamua hatma ya nchi hiyo baada ya jeshi kupuuza makataa ya kurejesha madaraka kwa rais Mohammed Bazoum kufikia Jumapili iliyopita.

Wafuasi wa Baraza la kitaifa la kulinda nchi ya Niger (CNSP) wakipeperusha bendera za Urusi walipokuwa wakiandamana mjini Niamey mnamo Agosti 6, 2023.  (Photo by AFP)
Wafuasi wa Baraza la kitaifa la kulinda nchi ya Niger (CNSP) wakipeperusha bendera za Urusi walipokuwa wakiandamana mjini Niamey mnamo Agosti 6, 2023. (Photo by AFP) AFP - -

Katika hatua nyingine, Mwanadiplomasia wa Marekani Victoria Nuland, amekutana na viongozi hao wa kijeshi, lakini akasema haoni matumaini ya jeshi kurejesha madaraka kwa rais Bazoum huku akisema mazungumzo hayo yalikuwa ya wazi, lakini magumu.

Akizungumza na RFI, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken, amesema njia bora ya kutatua mzozo wa Niger ni kwa njia ya kidiplomasia, huku Ufaransa nayo ikisema inaendelea kusimamia sera yake ya kurejesha madarakani uongozi uliochaguliwa kidemokrasia.

Tunaunga mkono juhudi za Ecowas kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger, hivyo tunashirikiana kidiplomasia na Ecowas. Tunawasiliana mara kwa mara na viongozi wa Afrika pamoja na washirika wetu wa Ulaya ikiwemo Ufaransa, mapinduzi haya yametuweka katika hali ngumu na kutulazimu kuweka vikwazo dhidi ya viongozi wa mapinduzi.

Wakati hayo yakijiri, uongozi wa kijeshi umteua Ali Mahaman Lamine Zeine kuwa Waziri Mkuu mpya.

Nchi ya Niger ni koloni la zamani la Ufaransa, na mapinduzi hayo yamesababisha wimbi la chuki dhidi ya Ufaransa na Urusi nchini humo, hali hii ikionekana kuwa sawa na hali ya majirani za Mali na Burkina Faso, ambazo zote zimeegemea Moscow tangu mapinduzi yao wenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.