Pata taarifa kuu

Niger: Viongozi wa Afrika Magharibi kukutana Alhamisi baada ya muda wao wa makataa kuisha

 Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) watakutana siku ya Alhamisi kujadili hali ya Niger wiki mbili baada ya mapinduzi na kumalizika kwa makataa yao siku ya Jumapili wakitaka kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba la sivyo watumie 'nguvu'.

Kanali-meja wa Amadou Abdramane, kutoka baraza la Ulinzi wa Kitaifa (CNSP) akilakiwa na waandamanaji alipowasili katika uwanja wa michezo wa Jenerali Seyni Kountché huko Niamey, Agosti 6, 2023.
Kanali-meja wa Amadou Abdramane, kutoka baraza la Ulinzi wa Kitaifa (CNSP) akilakiwa na waandamanaji alipowasili katika uwanja wa michezo wa Jenerali Seyni Kountché huko Niamey, Agosti 6, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo utafanyika Abuja, mji mkuu wa Nigeria inayoongozwa na Bola Tinubu, rais wa sasa wa ECOWAS.

Mnamo Julai 30, katika mkutano wa awali huko Abuja, viongozi wa Afrika Magharibi walitoa makataa ya wiki moja kwa wanajeshi ambao walichukua mamlaka huko Niamey kumrejesha Rais Mohamed Bazoum.

Huu utakuwa ni mkutano wa pili wa wakuu wa nchi kuitishwa chini ya wiki mbili, baada ya ule wa Julai 30. Kulingana na vyanzo vya RFI, nchi wanachama zimearifiwa na ujumbe kutoka kwa tume ya ECOWAS.

Ni mkutano uliopangwa mjini Abuja, katika nchi ya Bola Tinubu, rais wa Nigeria, mwenyekiti wa ECOWAS.

Mambo hayaendi jinsi jumuiya hiyo linavyotaka, huku majaribio ya upatanishi yakishindwa. Duru za kuaminika zinabaini kwamba, viongozi wa mapinduzi wanawasilisha kurejea kwa Rais Mohamed Bazoum kama kikwazo.

Mnamo Agosti 5, Bunge la Seneti la Nigeria pia lilisema haliungi mkono uingiliaji kati huo wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.