Pata taarifa kuu

ECOWAS: Uwezekano wa kumfungulia mashtaka rais Bazoum, ni 'aina mpya ya uchochezi'

Vitisho vya kesi za kisheria dhidi ya Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum kwa "uhaini mkubwa" vinajumuisha "aina mpya ya uchochezi" ambayo inapingana na "nia ya mamlaka ya kijeshi ya Jamhuri ya Niger kurejesha utulivu wa kikatiba kwa njia ya amani", Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imesema katika taarifa iliyotiwa saini mjini Abuja.

Jenerali Abdourahamane Tiani (kushoto) na Rais wa Niger Mohamed Bazoum (kulia).
Jenerali Abdourahamane Tiani (kushoto) na Rais wa Niger Mohamed Bazoum (kulia). © AP / AP - Ludovic Marin / Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Baada ya ECOWAS, Umoja wa Afrika umefanya mkutano kuhusu hali nchini Niger siku ya Jumatatu Agosti 14. Hatima ya rais aliyechaguliwa kidemokrasia bado haijulikani, hasa tangu CNSP ilipotangaza, jioni ya Jumapili Agosti 13, kwamba inataka kumfungulia mashtaka Mohamed Bazoum kwa "uhaini mkubwa" na "kuhatarisha usalama wa nchi", ikiwa ni "uchochezi mpya ”, kulingana na ECOWAS.

ECOWAS imesema, siku ya Jumatatu hii jioni, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, kuwa "imepokea kwa mshangao" tangazo hili la serikali ya kijeshi kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria rais aliyepinduliwa madarakani Julai 26.

Kwa mujibu wa ECOWAS, mtazamo huu unajumuisha "aina mpya ya uchochezi na inakinzana na dhamira inayohusishwa na mamlaka za kijeshi kurejesha utulivu wa kikatiba kwa njia za amani" na inalaani, kwa mara nyingine tena, kuzuiliwa kinyume cha sheria kwa Mohamed Bazoum na kutaka kuachiliwa kwake mara moja.

Katika hotuba iliyorushwa Jumapili jioni, msemaji wa CNSP alisema yuko na "uthibitisho wa mazungumzo" kati ya Mohamed Bazoum na "raia" bila kusahau "wakuu wa nchi na maafisa wa kigeni", kulingana na viongoziwa mapinduzi, "kushtaki mbele ya mamlaka za kitaifa na kimataifa rais aliyeondolewa madarakani na wapambe wake".

Utawala wa kijeshi utapendelea kumfikisha Mohamed Bazoum mbele ya sheria kwa "uhaini mkubwa" na "kuhatarisha usalama wa nchi" lakini inabakia kuamuliwa hasa ni aina gani za mashtaka zinaweza kuanzishwa na kwa misingi gani ya kisheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.