Pata taarifa kuu

Niger: Umoja wa Afrika waonyesha 'uungaji wake mkono thabiti' kwa ECOWAS

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika ameelezea leo Ijumaa Agosti 11, 2023 "wasiwasi wake mkubwa" kuhusu "kuzorota kwa mazingira ya kuzuiliwa" kwa rais wa Niger Mohamed Bazoum, akitaja "kutokubalika" matibabu yake na mamlaka ya kijeshi ambayo yalimpindua madarakani Julai 26. 

Moussa Faki Mahamat, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, wakati wa mahojiano yake na RFI pamoja na France 24, Novemba 19, 2022.
Moussa Faki Mahamat, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, wakati wa mahojiano yake na RFI pamoja na France 24, Novemba 19, 2022. © RFI / France 24
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa hiyo, Moussa Faki Mahamat "anaonyesha uungaji wake mkono thabiti kwa maamuzi ya ECOWAS", Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ambayo iliamua Agosti 10, 2023 kupeleka "kikosi wanajeshi kurejesha utawala wa kikatiba nchini Niger.

Umoja wa Afrika (AU) unaunga mkono Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuhusu hali nchini Niger.

Mnamo Agosti 10, 2023, mwishoni mwa mkutano wa kilele wa ECOWAS, wakuu wa nchi na serikali wa jumuiya hiyo walipaza sauti dhidi ya viongozi wa mapinduzi nchini Niger waliochukuwa madaraka kwa nguvu huko Niamey mnamo Julai 26. Waliamua kupeleka jeshi nchini Niger kurejesha utaratibu wa kikatiba.

Vikwazo vilivyowekwa pia vimedumishwa na vinapaswa kuimarishwa.

'Haraka kukomesha machafuko'

Shirika hilo hata hivyo limebainisha kwamba linaweka mezani chaguzi zote kwa ajili ya "suluhisho la amani" la mgogoro huo. Msimamo unaooungwa mkono katika ngazi ya bara, na Umoja wa Afrika.

Marais wa Afrika Magharibi wamedumisha vikwazo hivyo na kuweka wazi kuwa wanataka azimio la amani kwa njia ya mazungumzo. Lakini wakati huo huo waliamuru "kuweka tayari" vikosi vya kijeshi na kuvipeleka "kwa lengo la kurejesha utulivu wa kidemokrasia nchini 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.