Pata taarifa kuu

Niger: Wasiwasi waongezeka kuhusu mustakabali katika mzozo wa mapinduzi

NAIROBI – Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Marekani zimepaza sauti kuhusu hali ya rais Mohamed Bazoum, aliyeondolewa madaraka na jeshi la Niger Julai 26, wakati huu Jumuiya ya nchi za ECOWAS, zikiagiza jeshi kuwa tayari kurejesha uongozi wa kidemokrasia.

Rais Mohammed Bazoum
Rais Mohammed Bazoum © Niger Presidency
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya kigeni Josep Borrell, amesema amepata taarifa kuwa, rais Bazoum amenyimwa chakula, anaishi kwenye chumba kisichokuwa na umeme na amenyimwa huduma ya matibabu.

Umoja wa Afrika nao umesema, anachopitia rais Bazoum aliyechaguliwa kidemokrasia  hakikubaliki kamwe, na anapaswa kuachiwa huru.

Ebba Kalondo ni msemaji wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Rais wa tume ya Umoja wa Afrika Musa Faki Mahamat ameunga mkono maamuzi yote ya ECOWAS ya Agosti 10,2023 na pia ameonyesha wasiwasi wake kuhusu mazingira mabaya anamoishi rais Mohammed Bazoum. Kumtendea hivyo rais aliyechaguliwa kidemokrasia haikubaliki, hivyo ametoa wito wa kuachiwa huru mara moja kwa rais Bazoum.

Taarifa za ndani zinasema, licha ya Bazoum kuwa salama, hali yake sio nzuri, wakati huu jeshi la Niger likionya dhidi ya mpango wa jeshi la ECOWAS kuinglia mzozo huo baada ya hatua hiyo kukubaliwa kwenye mkutano wakuu w anchi waliokutana siku ya Alhamisi jijini Abuja, kama anavyoeleza Omar Touray, rais wa Tume  ya ECOWAS.

Baada ya juhudi zote za ECOWAS kutumia diplomasia kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger, tunaagiza kamati ya jeshi la ECOWAS kuunda kikosi cha dharura chenye uwezo mara moja kurejesha utawala wa kiraia.

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, baada ya mkutano huo alitaka jeshi la ECOWAS kutumwa haraka nchini  Niger.

Viongozi wote wa nje wanafikiri kuwa tumejaribu vya kutosha mazungumzo na uongozi wa kijeshi nchini Niger, tuwaambie viongozi hao wa kijeshi kuwa nafasi yao iko katika kambi za kijeshi, wanafaa kukabiliana na magaidi na sio kumteka rais ambaye amechaguliwa kidemokrasia. 

Licha ya shinikizo na vitisho kutoka ECOWAS na Jumuiya ya Kimataifa, wakuu wa jeshi nchini Niger wameendelea kupuuza wito huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.