Pata taarifa kuu

Niger : Wito wa kuachiwa kwa rais Bazoum waendelea kutolewa

Nairobi – Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Marekani zimepaza sauti kuhusu hali ya rais Mohamed Bazoum, aliyeondolewa madaraka na jeshi la Niger Julai 26, wakati huu Jumuiya ya nchi za ECOWAS, zikiagiza jeshi kuwa tayari kurejesha uongozi wa kidemokrasia. 

Taarifa za ndani zinasema, licha ya Bazoum kuwa salama, hali yake sio nzuri
Taarifa za ndani zinasema, licha ya Bazoum kuwa salama, hali yake sio nzuri AFP - STEFANO RELLANDINI
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya kigeni Josep Borrell, amesema amepata taarifa kuwa, rais Bazoum amenyimwa chakula, anaishi kwenye chumba kisichokuwa na umeme na amenyimwa huduma ya matibabu. 

Umoja wa Afrika nao umesema, anachopitia rais Bazoum aliyechaguliwa kidemokrasia hakikubaliki kamwe, na anapaswa kuachiwa huru. 

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, linasema limezungumza na Bazoum, daktari wake binafsi na wakili wa familia yake, siku ya Jumatano na Alhamisi na kuwaambia kuwa hajakutana na mtu tangu tarehe 4 mwezi huu, lakini pia haruhusiwi kukutana na familia yake. 

Taarifa za ndani zinasema, licha ya Bazoum kuwa salama, hali yake sio nzuri, wakati huu jeshi la Niger likionya kuwa litafanya mambo mabaya iwapo jeshi la ECOWAS litaingia nchini humo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.