Pata taarifa kuu

Bazoum anaendelea vema anakozuiwa na jeshi, ndugu zake wasema

Nchini Niger, aliyekuwa rais Mohamed Bazoum, aliyeondolewa madarakani na jeshi mwezi Julai, anaendelea vema kiafya pamoja na familia yake kwa mujibu wa ndugu zake.

Aliyekuwa rais wa Niger Mohamed Bazoum aliyeondolewa madarakani na jeshi mwezi Julai
Aliyekuwa rais wa Niger Mohamed Bazoum aliyeondolewa madarakani na jeshi mwezi Julai AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Hakikisho hili limetolewa siku chache, baada ya jeshi kudai kuwa, Bazoum, alikuwa anajaribu kutoroka kutoka katika eneo ambalo alikuwa amezuiwa tangu mwezi Julai.

Imebainika kuwa, Bazoum bado yupo jijini Niamey na mke wake na mtoto wa kiume ambao kwa kipindi chote wameendelea kuzuiwa pamoja.

Aidha, imeripotiwa kuwa Daktari wake amefanikiwa kumwona na hata kumletea chakula.

Kuhusu madai ya kuwa na mpango wa kutoroka nchi wiki hii, Wakili wake amekanusha madai hayo na kusema n ya uongo na kuongeza kuwa Bazoum ameendelea kuzuiwa bila ya kuwasiliana na watu wa nje.

Siku ya Ijumaa, rais wa Ufaransa Emmenuel Macron alisema, alikuwa na wasiwasi kuhusu hali ya Bazoum na kuendelea kushinikiza jeshi kumwachia huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.