Pata taarifa kuu
UFISADI-HAKI

Upinzani nchini Afrika Kusini unataka uchunguzi wa ufisadi ufanyike kwa makamu wa rais

Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini kimetoa wito siku ya Jumatatu kwa mamlaka kufanya uchunguzi kuhusu vitendo vya makamu wa rais wa nchi hiyo baada ya shutuma za ufisadi kwenye vyombo vya habari vya ndani na miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ambao uko hatarini kwa chama tawala.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha DA John Steenhuisen mnamo Desemba 13, 2022 katika Bunge la Afrika Kusini mjini Cape Town.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha DA John Steenhuisen mnamo Desemba 13, 2022 katika Bunge la Afrika Kusini mjini Cape Town. AP - Nardus Engelbrecht
Matangazo ya kibiashara

 

Kulingana na chunguzi kadhaa zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya Afrika Kusini, Paul Mashatile anaishi maisha ya anasa, akikaa hasa katika mali ya kifahari ya washirika wake wa karibu, badala ya upendeleo unaotolewa, miongoni mwa mambo mengine, katika muktadha wa mikataba.

"Tumetoa taarifa na tumetoa hati ya mashtaka," kiongozi wa Democratic Alliance (DA) John Steenhuisen amewaambia waandishi wa habari baada ya kuwasilisha kesi yake kwa polisi wa Cape Town. "Tutaendelea kutumia njia zote tulizonazo kuhakikisha kwamba haki inatendeka na kwamba suala hilo linachunguzwa ipasavyo," ameongeza.

Ukoo wa Mashatile haukujibu maombi ya maoni. Paul Mashatile katika wiki za hivi karibuni alikanusha shutuma za wazi za hatua za awali kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa makamu wa rais, ambao amekuwa akishikilia tangu mwezi Machi 2023. Mwezi uliopita chama cha DA kiliomba kwamba Rais Cyril Ramaphosa, ambaye aliahidi kutokomeza rushwa, amuachishe kazi mshirika wake wa karibu, na msiri wake.

"Shirika au mtu yeyote aliye na taarifa kuhusu uhalifu au vitendo vya kukemea" anaalikwa "kuwasilisha taarifa hii kwa polisi," amejibu msemaji wa rais, Vincent Magwenya.

Raia wa Afrika Kusini hivi karibuni wataitwa kwenye uchaguzi wa kulifanyia upya Bunge lao, ambalo litamteua rais ajaye. Tarehe kamili ya uchaguzi bado haijatangazwa, lakini inatarajiwa kati ya mwezi Mei na Agosti.

Kulingana na kura za maoni, ANC, inayokabiliwa na kesi za ufisadi na kulemewa na mazingira ya kijamii na kiuchumi, ina hatari ya kupoteza wingi wake kamili katika Bunge kwa mara ya kwanza katika historia yake. Sehemu ya upinzani ilikusanyika karibu na DA, ambayo iliunda muungano na vyama kumi vidogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.