Pata taarifa kuu

Niger: ECOWAS kukutana mjini Accra kujadili uwezekano wa mpango wa hatua ya kijeshi

Baada ya kuahirishwa Agosti 12, mkutano wa wakuu wa majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) hatimaye unafanyika Alhamisi hii, Agosti 17 huko Accra, Ghana. Wanakutana kwa siku mbili na watalazimika kukamilisha mpango wa uwezekano wa kuingilia kijeshi kurejesha utulivu wa kikatiba nchini Niger. Lakini chaguo hili lina udhaifu kadhaa.

Mji mkuu wa Ghana, Accra.
Mji mkuu wa Ghana, Accra. Creative Commons/Guido Sohne
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo utafanyika katika Kambi ya Burma huko Accra, makao makuu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Wanajeshi la Ghana. Mbali na wakuu wa majeshi, Kamishna wa Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama wa ECOWAS, Abdel Fatau Moussa, raia wa Ghana, atashiriki mkutano huo. Alikuwepo kwenye mkutano ulioidhinisha kikosi cha dharura cha ECOWAS, mwanzoni mwa mwezi Agosti huko Abuja. Kulingana na habari zetu, mkutano huo utahusu zaidi kukamilisha mpango wa kuingilia kijeshi nchini Niger, anabaii Jean-Luc Aplogan kutoka Cotonou.

Kuhusu kukusanywa na kupelekwa kwa vitengo vya wanajeshi, idadi ya nchi zinazochangia kama vile Senegal, Benin, Côte d'Ivoire na Nigeria sasa inajulikana kwa usahihi. Inabakia kupanga harakati zao kwenye maeneo watakapowekwa na kuhalalisha kwa uhakika njia ambayo wanajeshi wa nchi ambazo hazina mpaka na Niger watachukua.

Hata kama chaguo la kidiplomasia bado linawezekana na hata kutiwa moyo na baadhi ya watu mashuhuri katika siku za hivi karibuni, afisa mkuu wa kikosi cha dharura cha ECOWAS anaarifu kwamba makao ya jeshi la kikanda hayajapokea amri ya kupinga kutoka kwa ECOWAS. Kwa vyovyote vilei, "kuundwa na kutumwa kwa kikosi" bado ni muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.