Pata taarifa kuu

Niger yawaita nyumbani mablozi wake kutoka Ivory Coast na Nigeria

Viongozi wa kijeshi nchini Niger, wamewaita nyumbani mabalozi wake katika nchi za Ivory Coast na Nigeria, baada ya matamshi ya rais Alassane Ouattara, kuwa wanadiplomasia hao wanaunga mkono uvamizi wa kijeshi kwa nchi yao.

Utawala wa kijeshi unasema matamshi ya rais  Ouattara yalikuwa yanapongeza matumizi ya kijeshi dhidi yao
Utawala wa kijeshi unasema matamshi ya rais  Ouattara yalikuwa yanapongeza matumizi ya kijeshi dhidi yao © Stringer / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa kijeshi unasema matamshi ya rais  Ouattara yalikuwa yanapongeza matumizi ya kijeshi dhidi yao.

Rais Ouattara alikuwa amezungumzia kuhusu suala la kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kidemokrasia na rais aliyechaguliwa  Mohamed Bazoum.

Pia alikuwa amesema operesheni ya kijeshi kurejesha demokrasia nchini Niger inapaswa kuanza "haraka iwezekanavyo".

Kiongozi huyo alisema  Ivory Coast itachangia kati ya wanajeshi 850 na 1,100, pamoja na mataifa ya Nigeria na Benin.

Jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi Ecowas imesisitiza kufanyika kwa mazunguzmo na kutatua changamoto zilizoko kwa njia ya kidiplomasia lakini inasema uingiliaji kati wa kijeshi bado uko mezani.

Umoja huo ulisema kuwa ulishangazwa na hatua kwamba viongozi hao wa mapinduzi wameamua kuendeleza mashtaka dhidi ya  Bazoum kwa kile wanachosema ni uhaini mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.