Pata taarifa kuu

Mali na Urusi zatoa wito wa suluhu "kwa njia amani pekee" kwa mgogoro nchini Niger

Mkutano wa kijeshi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) utafanyika Alhamisi Agosti 17 na Ijumaa Agosti 18 nchini Ghana, kujadili uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini Niger na kumrejesha mamlakani rais Mohamed Bazoum ambaye alitimuliwa kupitia mapinduzi ya kijeshi. Wakati huo huo, Urusi na Mali zimetoa wito Jumanne, Agosti 15, kupitia sauti ya marais wao, kusuluhisha mgogoro huo "kwa njia ya amani ya kisiasa na kidiplomasia".

Kiongozi wa Mali Assimi GoΓ―ta (kushoto) na rais wa Urusi Vladimir Poutine (kulia) wamezungumza kwa njia ya simu kuhusu Niger, kulingana na Kremlin. Hapa, ilikuwa katika mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika huko Saint Petersburg mnamo Julai 29, 2023.
Kiongozi wa Mali Assimi GoΓ―ta (kushoto) na rais wa Urusi Vladimir Poutine (kulia) wamezungumza kwa njia ya simu kuhusu Niger, kulingana na Kremlin. Hapa, ilikuwa katika mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika huko Saint Petersburg mnamo Julai 29, 2023. Β© Mikhail Metzel/TASS via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Moscow, Anissa El Jabri

Mazungumzo haya ya simu kati ya Moscow na Bamako yamefanyika "kwa juhudi za Mali", imebainisha huduma ya vyombo vya habari ya Kremlin. Katika taarifa, ikulu ya Kremlin imebaini kwaba marais wa Urusi Vladimir Putin na Mali Assimi GoΓ―ta "wamesisitiza umuhimu wa kutatua hali kuhusu Jamhuri ya Niger kwa njia ya amani ya kisiasa na kidiplomasia".

Saa chache baadaye, katika mkutano wa 11 wa usalama wa kimataifa kuhusu Moscow - mkutano ulioandaliwa na jeshi la Urusi - Waziri wa Ulinzi wa Mali ameonyesha msimamo wako. Bila kumtaja jina, lakini kwa matamshi ya uwazi, Sadio Camara ameikosoa vikali ECOWAS:

"Uzembe wa mashirika ya kikanda, kutokuwa na uwezo wa kupata suluhisho, lakini haraka ya kulaani, kutishia, vikwazo, hata kushambulia kijeshi watu huru, inapelekea kuundwa kwa aina mpya za ushirikiano kulingana na mtazamo mbalimbali. "

Chini ya wiki tatu baada ya mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika mjini Saint Petersburg, mkutano huu kuhusu usalama wa kimataifa unakaribisha rasmi zaidi ya wageni 800 kutoka nchi 76, lakini hakuna wajumbe wa kijeshi kutoka nchi za Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.