Pata taarifa kuu

Niger: Wanajeshi wachache ndio wanaohusika na mapinduzi

Nairobi – Waziri wa mambo ya nje wa Niger, Hassoumi Massoudou, akizungumza katika mahojiano maalumu na idhaa ya RFI na France24 mjini Abuja Nigeria, amesema wanajeshi waliompindua rais Mohamed Bazoum, wanamtumia kutaka kuhalalisha mapinduzi waliyoyafanya dhidi ya demokrasia.

Waziri wa mambo ya nje wa Niger, Hassoumi Massoudou
Waziri wa mambo ya nje wa Niger, Hassoumi Massoudou © AFP/Pool
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka Nigeria wanaojaribu kusuluhisha mzozo wa Niger, wanasema utawala wa Kijeshi kwenye taifa hilo, uko tayari kutafuta muafaka kwa njia ya diplomasia, wakati huu ukivutana na jumuiya ya ECOWAS.

Kiongozi wa ujumbe wa  huo Sheikh Bala Lau ,uliokutana na uongozi wa kijeshi ,Niamey , ambapo akizungumza baada ya kikao hicho ,amesema jenerali Abdourahamane Tiani yuko tayari kwa mazungumzo ya kusaka suluhu.

Ecowas ilikuwa imetishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger
Ecowas ilikuwa imetishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger AFP - -

Hata hivyo, Tiani amesisitiza mapinduzi aliyoyaongoza yalikiwa na nia njema na yalilenga kukwepusha janga ambalo lingeathiri nchi jirani ikiwemo Nigeria.

“Kuna kikundi kidogo cha wanajeshi ambacho kimeamua kumfanya mateka rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ili kumtumia kuendelea kutawala.” alisema Hassoumi Massoudou.

00:30

Hassoumi Massoudou kuhusu kutekewa kwa rais wa Niger

Aidha Massoudou aliwasifu waandamanaji waliojitokeza mjini Niamey kupinga utawala wa kijeshi.

“Katika nchi haikubaliki kila siku maandamano, kunayo maandamano Niamey ambapo watu wanapigwa risasi. Siku ya mapinduzi yalizuka maandamano ambapo watu walipigwa risasi.” alieleza Hassoumi Massoudou.

00:31

Hassoumi Massoudou kuhusu maandamano Nigerr

Katika hatua nyingine, Hassoumi Massoudou, amesisitza kuwa uvamizi wa kijeshi wan chi za ECOWAS hautamaanisha vita dhidi ya taifa hilo bali kurejesha utawala wa sheria.

Viongozi wa kijeshi nchini Niger, wamewaita nyumbani mabalozi wake katika nchi za Ivory Coast na Nigeria, baada ya matamshi ya rais Alassane Ouattara, kuwa wanadiplomasia hao wanaunga mkono uvamizi wa kijeshi kwa nchi yao.

Uongozi wa ECOWAS umetaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia  nchini Niger
Uongozi wa ECOWAS umetaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Niger © AFP/Kola Sulaimon

Kwa upande mwengine, wabunge wa upinzani nchini Ghana, wameonesha kuguswa na mapendekezo ya viongozi wa Ecowas kuhusu uwezekano wa kuivamia kijeshi Niger, wakimtaka rais Nana Akufo-Addo, asitishe mpango wa kutuma wanajeshi wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.