Pata taarifa kuu

Niger: Wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la AU watafautiana kuhusu vikwazo vya ECOWAS

Jumuiya ya kimataifa yafuatilia hali nchini Niger tangu mapinduzi ya Julai 26. Taarifa ya mwisho kuhusu mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC), ambao ulifanyika Addis Ababa mnamo Agosti 14, 2023, bado inasubiriwa. Suala la vikwazo vilivyoamuliwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi dhidi ya Niger halikuweza kuafikiwa ndani ya PSC, kama wanadiplomasia wa Afrika walivyoielezea RFI.

Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa.
Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa. RFI/David Kalfa
Matangazo ya kibiashara

Mkutano "mgumu", ", na "mrefu " kimebaini chanzo cha kidiplomasia cha Kiafrika ambacho kinaona ndani yake ishara ya ufahamu wa nchi wanachama juu ya hali ambayo haijawahi kutokea. "Kumekuwa na mapinduzi sita katika kipindi kisichozidi miaka mitatu" katika bara hilo, kinakumbusha chanzo hiki.

Athari: "Tuko mbele ya hali ambayo katiba zetu haziendani tena" na mikutano ya Baraza la Usalama la Amani, inazidi kuwa "migumu" , chanzo hiki kimesema.

Kwa mujibu wa chanzo hiki, kiini cha mijadala hiyo kilijikita katika msimamo wa Umoja wa Afrika kuhusiana na maamuzi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS). "Baadhi, ndani ya Baraza, walitamani, kuweza kueleza kutoridhishwa na kuomba ufafanuzi zaidi katika mlolongo ambao unaweza kusababisha" kwa chaguo la kuinilia kijeshi lililopendekezwa na ECOWAS, amebainisha,.

Nchi wanachama wa CSP zimekuwa zikijadiliana tangu Agosti 14 kuhusu masharti kamili ya taarifa ya mwisho.

Kwa upande wake, mwanadiplomasia mwingine wa Kiafrika, aliyeshiriki katika mkutano huo, anasema kuwa nchi za kusini mwa Afrika na Afrika Kaskazini "zinapinga uingiliaji wowote wa kijeshi". Nchi za Afrika ya Kati, kulingana na chanzo hiki, pia zimeelezea kutokubaliana na hatua chaguo hili la kuingilia kijeshi nchini Niger.

Mwishoni mwa mkutano huo, maandishi ya tamko hilo yaliwekwa "kapuni" kwa maneno ya mmoja wa wanadiplomasia hao. Nchi wanachama wa Baraza la Amani na Usalama zimekuwa zikijadiliana masharti yake halisi tangu Agosti 14. Kwa sababu ni hati ambayo "inatuhusu sote", kimekumbusha chanzo chetu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.