Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Nigeria: Gavana wa Benki Kuu akamatwa, baada ya kusimamishwa kazi

Rais mpya wa Nigeria Bola Tinubu alimsimamisha kazi gavana wa benki kuu - CBN - usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi Juni 10. Godwin Emefiele, mshirika wa karibu wa rais wa zamani Muhammadu Buhari, anawajibika hasa kwa uhaba mkubwa wa pesa ambao ulizorotesha uchumi wa Nigeria mwanzoni mwa mwaka. Sera yenye utata ya fedha iliyolenga kuchukua nafasi ya noti zote za nchi ilikuwa imesababisha mgogoro huu mkubwa wa ukwasi. Lakini uamuzi huu unakosolewa na upinzani.

Mkuu wa Benki Kuu ya Nigeria Godwin Emefiele amesimamishwa kazi na kisha kukamatwa.
Mkuu wa Benki Kuu ya Nigeria Godwin Emefiele amesimamishwa kazi na kisha kukamatwa. © REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Lagos, Liza Fabbian

Baada ya miaka tisa katika uongozi wa Benki Kuu ya Nigeria, Godwin Emefiele amesimamishwa kazi na kukamatwa na vyombo vya usalama vya Nigeria. Idara ya Usalama ya jimbo ilithibitisha Jumamosi alasiri kwamba alikuwa ameshikiliwa na huduma zake.

Video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha Godwin Emefiele akipanda ndege binafsi, achini ya uangalizi wa wanaume kadhaa waliovalia suti, huku akifungwa pingu mkononi.

Taarifa ya serikali iliyotolewa usiku wa Ijumaa ilisema kuwa gavana wa CBN amesimamishwa kazi kufuatia uchunguzi unaoendelea. Godwin Emefiele huenda alikosolewa vikali, lakini kusimamishwa huku kunazua maswali ya kisheria.

Gavana wa enki kuu ya taifa, CBN, Godwin Emefile na rais Muhammadu Buhari kama Mwenyekiti wazindua noti mpya za Naira na kuongoza mkutano wa FEC katika Ikulu ya Abuja.
Gavana wa enki kuu ya taifa, CBN, Godwin Emefile na rais Muhammadu Buhari kama Mwenyekiti wazindua noti mpya za Naira na kuongoza mkutano wa FEC katika Ikulu ya Abuja. © Sunday Aghaeze>2022/ Arise News

Chama cha Labour kinamtuhumu mkuu mpya wa nchi kwa kufanya 'uchunguzi' wa kibinafsi dhidi ya Godwin Emefiele - anayeshutumiwa kwa kuvuruga kampeni ya uchaguzi kwa kuchukua nafasi ya noti zote za Nigeria, akionekana kupambana dhii ya ununuzi wa kura.

Mnamo mwaka wa 2014, kufutwa kazi kwa Sanusi Lamido Sanusi, ambaye wakati huo alikuwa gavana wa Benki Kuu, na Rais Goodluck Jonathan kulisababisha kashfa nchini Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.