Pata taarifa kuu

Tinubu aapishwa kuwa rais mpya wa Nigeria

NAIROBI – Bola Tinubu ameapishwa kuwa rais mpya wa Nigeria, akimrithi rais anayeondoka kwa sasa Muhammadu Buhari, anayemaliza hatamu yake.

Bola Tinubu, Rais mpya wa Nigeria
Bola Tinubu, Rais mpya wa Nigeria © AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Tinubu mwenye umri wa miaka 71 anayetokea kusini mwa Nigeria, anachukua uongozi wa taifa hilo la Afrika wakati huu linapokabiliwa na changamoto za kiuchumi na ukosefu wa usalama unaotekelezwa na Makundi ya watu wenye silaha.

Wakati akila kiapo Bola amesema kwamba atatekeleza majukumu yake kwa raia wa Nigeria kwa uadilifu na uaminifu kwa manufa ya wote wakiwemo waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura.

Viongozi wa kigeni na wawakilishi wa serikali waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na rais wa Afrika Kusini  Cyril Ramaphosa, Paul Kagame wa Rwanda na Nana Akufo-Addo wa Ghana na wajumbe kutoka nchi za Marekani , Uingereza na China.

Kashim Shettima ameapishwa kuwa naibu wa rais wa rais akichukua nafasi ya Yemi Osinbajo.

Tinubu wa chama tawala alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa tarehe 25 mwezi Februari baada ya kupata kura milioni 8.8 na kuafikia vigezo vinavyohitajika kabla ya kutangazwa rais.

Kiongozi wa upinzani Atiku Abubakar, aliyemaliza katika nafasi ya pili pamoja na Peter Obi, alichukua nafasi ya tatu wamewasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Tinubu mahakamani kwa misingi kuwa uchaguzi huo uligubikwa na udaganyifu.

Tinubu alikuwa gavana wa jimbo la  Lagos kati ya mwaka wa 1999  hadi  2007, kipindi ambacho wafuasi wake wanasema alitekeleza mageuzi makubwa katika sekta ya biashara.

Licha ya hao, anakabiliwa na shutuma za ufisadi, madai ambayo ameyakana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.