Pata taarifa kuu

Wakuu wa nchi za Afrika wanahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Tinubu Nigeria

NAIROBI – Baadhi ya viongozi wa bara Afrika na wajumbe kutoka nchi za kigeni wamewasili nchini Nigeria kwa hafla ya kuapishwa kwa Bola Tinubu kuwa rais wa 16 wa taifa hilo.

Wakuu wa nchi za Afrika wanahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Bola Tinubu nchini Nigeria
Wakuu wa nchi za Afrika wanahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Bola Tinubu nchini Nigeria © Ikulu ya Afrika Kusini
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, karibia viongozi ishirini kutoka nchi za barra Afrika wanatarajiwa kuhuduria sherehe hizo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ni miongoni wa viongozi waliowasili mjini Abuja siku ya Jumapili.

Tayari marais ambao wako nchini Nigeria ni pamoja na rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, rais wa Congo Brazzaville, Denis Sassou Nguesso, rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embaló na Julius Maada Bio wa Sierra Leone.

Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, rais wa mpito wa Chad Mahamat Déby, kiongozi wa wa Niger, Mohamed Bazoum na rais Nana Akufo-Ado wa Ghana pia não wanahudhuria hafla hiyo nchini Nigeria.

Mkuu wa mawaziri wa nchini Kenya, Musalia Mudavadi, anawakilisha rais William Ruto.

Ujumbe wa watu tisa kutoka Marekani na maofisa wa China wakiongozwa na mwanachama mkuu wa Chama cha Kikomunisti pia wamewasili kwa ajili ya hafla hiyo.

Ushindi wa Tinubu katika uchaguzi wa urais uliopita unapingwa na wapinzani wake.

Siku ya Jumanne, mahakama itaanza kusikiliza hoja kuu katika ombi la uchaguzi.

Tinubu anatarajiwa kuchukua madaraka kutoka kwa rais Muhammadu Buhari ambaye amekuwa akiongoza tangu mwaka 2015.

Katika hotuba ya kuwaaga raia wa nchi yake, Buhari anaiacha Nigeria ikiwa nchi bora kinyume na alivyoipokea.

Wakati Buhari akiondoka, changamoto kubwa zinazomkabili kiongozi mpya ni usalama hasa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo na suala la uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.