Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Washington yasikitishwa na ukiukaji wa usitishaji mapigano nchini Sudan

Marekani imesema inasikitihwa na 'ukiukaji' wa usitishaji mapigano nchini Sudan, ikitoa wito kwa jeshi na wanamgambo kuheshimu makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyoanza kutekelezwa siku ya Jumatatu jioni.

Moshi ukifumba juu ya majengo katika mji mkuu wa Sudan Khartoum mnamo Mei 24, 2023.
Moshi ukifumba juu ya majengo katika mji mkuu wa Sudan Khartoum mnamo Mei 24, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Tunaendelea kushuhudia ukiukaji wa usitishaji mapigano" hasa katika miji ya Khartoum na Darfur, magharibi mwa nchi, ikiwa ni pamoja na mizinga, ndege za kivita na ndege zisizo na rubani, amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Matthew Miller.

"Tunashinikiza pande husika kwa madai ya ukiukaji huu," amewaambia waandishi wa habari, akisisitiza kwamba Marekani ina haki ya kuweka vikwazo "ikiwa ni lazima". Hata hivyo, amekataa kuzungumzia ratiba au nani atakayelengwa na vikwazo hivi.

Rais wa Marekani Joe Biden alitia saini agizo mapema mwezi Mei la kuimarisha mamlaka ya serikali ya Marekani kuweka vikwazo dhidi ya "watu wanaotishia amani, usalama na utulivu wa Sudan; wanaodhoofisha kipindi cha mpito cha demokrasia; wanaotumia vurugu dhidi ya raia; na wanaofanya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu."

Jeshi na wanamgambo wanaowania madaraka nchini Sudan walishutumiana siku ya Alhamisi kwa kuvunja mapatano yaliyojadiliwa na wapatanishi wa Marekani na Saudi Arabia.

Vita vilivyozuka Aprili 15 vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,800, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la ACLED, watu zaidi ya milioni moja wameyahama makazi yao na wengine zaidi 300,000 wameitoroka nchi hiyo, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.