Milio ya risasi imesikika Sudan kuelekea utekelezwaji wa mktaba wa kusitisha vita
NAIROBI – Milio ya risasi na milipuko kwa mara nyingine imeshuhudiwa nchini Sudan hivi leo, saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mktaba wa kusitisha mapigano kwa wiki moja ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia walio katika maeneo yalioathirika na vita hivyo.
Imechapishwa:
Makabliano haya mapya yanaripotiwa licha ya makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano ambayo yalikosa kuheshimiwa, ya hivi punde ikiwa mkabata ulioafikiwa kati ya pande mbili zinazopigana chini ya usimamizi wa Marekani na Saudi Arabia.
Kulingana na Marekani na Saudi Arabia, mkataba wa hivi punde ulioafikiwa siku ya Jumapili unafaa kuanza kutekelezwa Jumatatu ya wiki hii usiku ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.
Siku ya Jumapili, pande hizo mbili zilitoa hakikisho la kuheshimu makubaliano haya mapya, hatua ambayo ilikaribishwa na Umoja wa mataifa, umoja wa Afrika, Jumuiya za kikanda, Afrika mashariki na IGAD.
Licha ya makubaliano kadhaa ya usitishaji ya hapo awali kukosa kuheshimiwa, raia wa nchi hiyo walikuwa na matumaini kwamba mkataba huu mpya utatoa fursa ya kumaliza vita ambavyo vimeitikisa Khartoum na sehemu zingine nchini humo.
Takriban watu elfu 1 wameripotiwa kuuawa huku maelfu wakikimbia vita hvyo, wakati huu pia madaktari katika mji wa Khartoum wakionya juu ya kuanguka kwa mfumo wa afya jijini Khartoum.