Pata taarifa kuu

Sudan: Mapigano yaripotiwa Khartoum, usitishaji mapigano kuanza Jumatatu

Kumeripotiwa mapigano zaidi kwenye jiji la Khartoum nchini Sudan, licha ya tangazo la Serikali ya Saudi Arabia na Marekani, kudai kuwa wamefanikiwa kuzishawishi pande hasimu kusitisha mapigano kwa wiki moja.

Wanajeshi wa Sudan wakiwa wamesimama jirani na gari lao katika moja ya kizuizi mjini Khartoum. May 20, 2023.
Wanajeshi wa Sudan wakiwa wamesimama jirani na gari lao katika moja ya kizuizi mjini Khartoum. May 20, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano ya kusitisha mapigano, yametiwa saini na wawakilishi wa jeshi na wale wa wapiganaji wa RSF, baada ya mazungumzo ya mjini Jeddah na sasa yataanza kutekelezwa rasmi kuanzia siku ya Jumatatu.

 

Chini ya makubaliano haya, mbali na usitishwaji wa mapigano, pande hizo mbili zitatakiwa kutuhusu kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu kwa raia walionaswa kwenye mapigano.

 

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema, haifahamiki ikiwa mkuu wa majeshi ya Sudan jenerali Abdel Fattah al Burhani na mwenzake anayeoongoza kundi la RSF Mohamed Dagalo, watakuwa tayari kuheshimu makubaliano ya safari hii.

 

Haya yanajiri wakati huu umoja wa Mataifa ukisema hadi kufikia mwishoni mwa juma hili, watu zaidi ya milioni 1 na laki moja wamekimbia makazi yao na wengine kuwa wakimbizi kwenye nchi jirani.

 

Tangu awali mahasimu hawa wawili wamekuwa wakisisitiza kuendelea na vita, kila mmoja akidai kuwa lengo lake ni kuibuka mshindi katika vita ya kuwania madaraka yanyoendelea na ambapo imeingia wiki ya 6.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.