Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Wanafunzi kumi watekwa nyara kaskazini magharibi mwa Nigeria

Wanafunzi kumi wa shule ya upili hawajulikani waliko tangu siku ya Jumatatu, baada ya kutekwa nyara katika jimbo la Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria, eneo lililoshuhudia visa vingi vya utekaji nyara kwa wanafunzi miaka iliyopita, mamlaka imesema leo Jumanne.

Huu ni utekaji nyara wa kwanza wa wanafunzi katika mkoa huo baada ya kipindi cha utulivu, hasa tangu serikali ya shirikisho kuanza kusambaza noti mpya ili kukomesha malipo ya fidia kwa watekaji nyara kabla ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa Februari.
Huu ni utekaji nyara wa kwanza wa wanafunzi katika mkoa huo baada ya kipindi cha utulivu, hasa tangu serikali ya shirikisho kuanza kusambaza noti mpya ili kukomesha malipo ya fidia kwa watekaji nyara kabla ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa Februari. © REUTERS/Bosan Yakusak
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi kumi wa shule ya sekondari ya umma ya Awon walitekwa nyara katika mazingira tatanishi, amesema Samuel Aruwan, Kamishna wa Usalama wa Ndani wa Jimbo la Kaduna.

Huu ni utekaji nyara wa kwanza wa wanafunzi katika mkoa huo baada ya kipindi cha utulivu, hasa tangu serikali ya shirikisho kuanza kusambaza noti mpya ili kukomesha malipo ya fidia kwa watekaji nyara kabla ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa Februari.

"Serikali ya Jimbo la Kaduna imepokea ripoti za awali kutoka kwa vyombo vya usalama juu ya kutekwa kwa wanafunzi karibu kumi," Aruwan amesema katika taarifa. Haijajulikana ikiwa wanafunzi wametekwa nyara kutoka shuleni au njiani wakienda shuleni, ameongeza. "Ripoti za kina zinazotarajiwa zitaelezea" mahali halisi pa tukio hilo.

Kaduna ni moja wapo ya majimbo mengi kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria yanayokabiliwa na magenge ya watu wenye silaha wanaoitwa "majambazi" ambao hushambulia vijiji, kuuwa raia na kujihusisha na utekaji nyaraili  kupata fidia. Katika miaka miwili iliyopita, mamia ya wanafunzi walitekwa nyara mashuleni, kama vile Kaduna.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.