Pata taarifa kuu

Mwanasiasa wa Nigeria apatikana na hatia ya njama ya kuvuna kiungo cha mwili

Mahakama jijini London nchini Uigereza, imempata na hatia aliyekuwa Naibu wa Seneta nchini Nigeria  kwa kupanga kununua figo ya mchuuzi kwa ajili ya binti yake anayeumwa. 

Mahakama iliwapata watatu hao na hatia ya kumsafirisha kijana mmoja hadi Uingereza kwa nia ya kutoa sehemu za mwili wake baada ya kesi ya wiki sita katika Old Bailey.
Mahakama iliwapata watatu hao na hatia ya kumsafirisha kijana mmoja hadi Uingereza kwa nia ya kutoa sehemu za mwili wake baada ya kesi ya wiki sita katika Old Bailey. AP
Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa huyo  Ike Ekweremadu,60, mkewe Beatrice, 56, na Daktari wao Obeta, 50, wamepatikana na hatia hiyo kwa kupanga kumdanganya mchuuzi huyo kutoka Lagos, ili kupata kiungo hicho cha mwili wake.

Hata hivyo, binti yake Sonia mwenye  umri wa miaka 25, amefutiwa mashtaka dhidi yake, baada ya uamuzi huo kutolewa baada ya saa 14.

Hii ndio mara ya kwanza kwa kesi kama hii kusikilizwa na kuamuliwa nchini Uingereza, tangu kupitishwa kwa sheria  mwaka 2015, inayopinga utumwa wa kisasa.

Nchini Uingereza, ni kosa kwa mtu kutoa figo yake kwa mgonjwa ili kupata malipo, na katika kesi hii Naibu Seneta huyo wa Nigeria, alimsafirisha mchuuzi huyo mwenye umri wa miaka 21 jijini London, ili atolewe kiungo hicho na angelipwa zaidi ya Dola Elfu nane.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu anayehusika na kosa hilo na kuthibitishwa atafungwa jela maisha. Baada ya  watatu hao kubainika kuteka kosa hilo, hukumu dhidi yao itatolewa tarehe 5 mwezi Mei.

Tangu 2003, Ekweremadu aliwakilisha eneo bunge la Enugu Magharibi kupitia chama cha Peoples Democratic Party, PDP, lakini katika uchaguzi uliopita, hakuwania kwa sababu alikuwa kizuizini.

Njama mbaya

Mwendesha mashtaka mkuu Joanne Jakymec amesema hii ni njama ya kutisha ya kumsafirisha mtu hadi Uingereza kwa lengo la kupandikiza figo yake.

Washtakiwa waliopatikana na hatia walionyesha kutojali kabisa afya na ustawi wa mwathiriwa, na walitumia ushawishi wao kwa kiwango cha juu, wakati muathiriwa akiwa na uelewa mdogo wa kile kinachoendelea. Amesema Jakymec.

Naye Inspekta Esther Richardson, kutoka kituo cha utumwa wa kisasa cha Metropolitan, amemsifia mwathiriwa kwa ushujaa wake dhidi ya wahalalifu hawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.