Pata taarifa kuu

Nigeria: Peter Obi amewasilisha kesi Mahakamani kupinga ushindi wa Tinubu

NAIROBI – Nchini Nigeria, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Leba, Peter Obi, amewasilisha kesi Mahakamani, kupinga ushindi wa aliyekuwa mgombea wa chama tawala cha APC Bola Tinubu, uliofanyika mwezi uliopita.

Peter Obi, kiongozi wa chama cha Leba nchini Nigeria amewasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Bola Tinubu
Peter Obi, kiongozi wa chama cha Leba nchini Nigeria amewasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Bola Tinubu AP - Mosa'ab Elshamy
Matangazo ya kibiashara

Hii sio mara ya kwanza kwa uchaguzi wa urais nchini Nigeria kupingwa Mahakamani, lakini upinzani haujawahi kushinda.

Wakati wa uchaguzi uliopita,Obi alimaliza katika nafasi ya tatu, mbele ya mgombea mkuu wa upinzani Atiku Abubakar wa chama cha PDP ambaye pia alipinga ushindi wa Tinubu.

Msemaji wa chama cha Leba Yunusa Tanko amesema, Obi amekwenda kupinga ushindi wa rais mteule, lakini pia namna Tume ya Uchaguzi ilivyoendesha zoezi la kukusanya matokeo ya urais na kuyantangaza.

Waangalizi wa Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikiri kutokea kwa hitilafu katika mfumo wa kusambaza matokeo kutoka vituoni, uliolenga kuzuia wizi wa kura.

Mahakama ya rufaa itaunda jopo maalum ambalo litakuwa na siku  180 kusikiliza na kuamua kesi hiyo.

Iwapo Obi na wapinzani wengine hawataridhika na uamuzi na jopo hilo, watakuwa huru kwenda katika Mahakama ya Juu ambayo itakuwa na siku 60 kusikiliza kesi hiyo.

Iwapo ushindi wa Tinubu, utathibitishwa na Mahakama, anatarajiwa kuapishwa Mei 29.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.