Pata taarifa kuu
UCHAGUZI - NIGERIA

Upinzani nchini Nigeria wapinga mahakamani ushindi wa rais Bola Tinubu

Nchini Nigeria, aliyekuwa mgombea mkuu wa upinzani wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliopita, Atiku Abubakar wa chama cha PDP, amewasilisha kesi Mahakamani kupinga ushindi wa Bola Tinubu wa chama tawala APC.

Makamu wa Rais wa zamani wa Nigeria, Atiku Abubakar
Makamu wa Rais wa zamani wa Nigeria, Atiku Abubakar © premium times
Matangazo ya kibiashara

Abubakar amewasilisha kesi kwenye Mahakama ya rufaa, baada ya aliyekuwa mgombe mwingine, Peter Obi, kutoka chama cha Leba, aliyeibuka katika nafasi ya tatu, naye kuwasilisha pingamizi kutaka ushindi wa Tinubu, kutupiliwa mbali.

Mwanasiasa huyo wa chama cha PDP aliyemaliza katika nafasi ya pili, katika shauri lake, amedai kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais sio halali, kwa sababu Tume ya Uchaguzi ilishindwa kuheshimu sheria za uchaguzi, kwa kuwekwa matokeo hayo kwenye tovuti yake.

Aidha, amedai kuwa Tinubu hakufikisha sharti la katiba, linalomtaka mshindi kupata wingi wa kura katika majimbo 24 kati ya 36 nchini humo.

Atiku Abubakar pia anataka atangazwe mshindi wa uchaguzi huo, au matokeo hayo yafutwa na uchaguzi mwingine ufanyike.

Mahakama ya rufaa itaunda jopo maalum ambalo litakuwa na siku  180 kusikiliza na kuamua kesi hiyo. Lakini iwapo Abubakar na Obi hawataridhika na uamuzi na jopo hilo, watakuwa huru kwenda katika Mahakama ya Juu ambayo itakuwa na siku 60 kusikiliza kesi hiyo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.