Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Wanajeshi kadhaa wauawa na wanajihadi magharibi mwa Chad

"Askari wengi" wameuawa leo Jumanne na wanajihadi walioshambulia kituo cha jeshi magharibi mwa Chad, msemaji wa ofisi ya rais ameliambia shirika la habari la AFP.

Wanajeshi wa Chad wakiwa kwenye magari yenye silaha wakati wa sherehe huko Ndjamena, Januari 2021.
Wanajeshi wa Chad wakiwa kwenye magari yenye silaha wakati wa sherehe huko Ndjamena, Januari 2021. AFP - RENAUD MASBEYE BOYBEYE
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo pia limesababisha "majeruhi", Brah Mahamat amesema katika taarifa yake. Shambulio hilo limetekelezwa "asubuhi na mapema" karibu na mji wa Ngouboua, katika eneo la Ziwa Chad, kwenye mipaka ya Chad, Niger, Cameroon na Nigeria, ambapo makundi ya wanajihadi ya Boko Haram na tawi lake lililojitenga la Islamic State katika Afrika Magharibi (Iswap) hushambulia mara kwa mara majeshi na raia katika nchi hizo nne.

Kikosi cha jeshi, "kilichotumwa kama mtangulizi wa kuanzisha kituo cha juu katika kisiwa cha Bouka-Toullorom", "kimeshambuliwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram", amebainisha Bw. Mahamat. 

"Wengi waliopoteza maisha na waliojeruhiwa wote ni wanajeshi wa vikosi vya ulinzi," msemaji wa ofisi ya rais ameliambia shirik la habari la AFP.

Ziwa Chad ni eneo kubwa la maji na vinamasi vilivyo na mamia ya visiwa, ambavyo vingine vinatumika kama maficho ya wanajihadi wa Boko Haram na Iswap. "Leo, Boko Haram hawana tena nguvu ya kushambulia kambi za jeshi" katika eneo la ziwa na sasa wanalenga "watu na mali zao," Rais wa Chad, Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, alisema siku 10 zilizopita, alipokuwa akizuru eneo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.