Pata taarifa kuu

Umoja wa Afrika waijadili Chad kufuatia mgogoro wa kisiasa unaoendelea

Tume ya Umoja wa Afrika, inayoshughulikia amani na usalama imeanza kikao kuhusu nchi ya Chad, wakati huu wanaharakati wa kisiasa katika  nchi hiyo ya Afrika ya Kati, wakishtumu Umoja huo, kwa kushindwa kuwachukulia hatua viongozi wa nchi yao, kufuatia mauaji ya wapinzani yanayoendelea

Vizuizi katika mitaa ya Ndjamena nchini Chad, wakati wa vurugu za Oktoba 20, 2022.
Vizuizi katika mitaa ya Ndjamena nchini Chad, wakati wa vurugu za Oktoba 20, 2022. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume hiyo yenye wanachama 15 inachunguza ripoti ya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki, ambaye pia ni raia wa Chad, anayetaka serikali ya mpito inayoongzwa na Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, kuwekewa vikwazo, hatua ambayo imeikarisha uongozi wa Chad. 

Mbali na malalamiko ya uongozi wa Chad kuwalenga wapinzani, hasa baada ya maafisa wa upinzani kuwapiga risasi waandamanaji mwezi Oktoba na kuwauwa watu zaidi ya 50, kiongozi wa nchi hiyo ameshtumiwa kwa kukataa kuheshimu makubaliano ya kuwa madarakani kwa kipindi cha mpito cha miezi 18 na kukabidhi madaraka kwa raia. 

Aidha, kwa mujibu wa ripoti hiyo, Faki anataka kuteuliwa kwa mjumbe maalum kutoka Umoja wa Afrika kufuatilia maendeleo ya kisiasa na usalama nchini Chad na kuhakikisha kuwa nchi hiyo inarejea kwenye misingi ya demokrasia. 

Haya yanajiri wakati huu, Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Kati, zikiwa zimemteua rais wa DRC Félix Tshisekedi kuongoza jitihada za kusuluhisha mvutano wa kisiasa nchini Chad. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.