Pata taarifa kuu

Chad: Kiongozi wa upinzani ataka uchunguzi wa ICC ufanyike kuhusiana na tukio la Oktoba 20

Mwanasiasa wa upinzani nchini Chad Succès Masra, ametoa wito kwa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, kuchunguza tukio la maafisa wa usalama kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji  tarehe 20 mwezi Oktoba na kusababisha vifo vya watu 50 na wengine zaidi ya 300 walijeruhiwa.

Kiongozi wa chama cha upinzani Les Transformateurs, Success Masra, mjini Ndjamena mnamo Mei 3, 2021.
Kiongozi wa chama cha upinzani Les Transformateurs, Success Masra, mjini Ndjamena mnamo Mei 3, 2021. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kiraia yanasema huenda idadi ya watu waliopoteza maisha ni kubwa, kushinda ile iliyotolewa. 

Wanasheria wa Succès Masra wanaamini kuwa dalili zilizowasilishwa kwao zinaonyesha kuwa uhalifu dhidi ya binadamu unafanywa nchini Chad na kwamba ICC ina uwezo wa kufungua uchunguzi. Kwa hivyo uhalifu huu, ni mbaya mno, kulingana na wakili Vincent Brengarth, wakili mwenza wa Succès Masra, ambaye anaamini kwamba ni muhimu "kuchukuwa hatua kali".

"Na kasi hii ya juu pia ni kikwazo ambacho jaji anaweza kutekeleza wakati ukweli ukidhihirika. Nadhani hatuwezi kuvumilia hali kuendelea na hatuwezi kuvumilia kwamba utawala wa kisiasa unaweza kudumishwa kwa kukandamiza upinzani, "amebaini.

Kulingana na mwanasheria huyo, ombi hili ni mwendelezo wa kimantiki wa miitikio ya jumuiya ya kimataifa. "Malalamiko mbalimbali na tahadhari mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na mashirika ya kimataifa, lakini pia na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa lazima pia ziwe na tafsiri yenye vikwazo zaidi na tafsiri hii ya kisheria ni nguvu ambayo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai inaweza kuwa nayo," amesema.

Anasema, uchunguzi wa ICC pia ungekuwa ujumbe: "Onyesha na uthibitishe tena kwa mamlaka ya Chad kwamba wana udhibiti wa karibu sana juu ya kile kinachotokea na kwamba hakuna kitu kinachoweza kuvumilia vitendo ambavyo vimekuwa kitekelezwa tangu sasa miezi kadhaa " .

'Lazima tutimize jukumu letu katika jamii'

Kwa upande wake, serikali ilikubali ujumbe wa kimataifa wa kutafuta ukweli juu ya matukio ya Oktoba 20. Na nchini humo, mashirika mengi yamekuwa yakijaribu kusaidiaraia kwa njia mbalimbali tangu vurugu za Oktoba 20, anaripoti mwandishi wetu maalum, Sébastien Nemeth.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.