Pata taarifa kuu

Chad: Mamlaka zatoa rasmi toleo lao la matukio ya Oktoba 20

Karibu wiki tatu baada ya tukio baya la umwagaji damu, Oktoba 20, ambapo kulingana na mamlaka nchini Chad, karibu watu hamsini walipoteza maisha, wakati wa maandamano dhidi ya taasisi za mpito, hatimaye serikali inatoa toleo lake kuhusiana na kilichotokea siku hiyo.

Huko Ndjamena, maandamano dhidi ya serikali yalishika kasi tarehe 20 Oktoba 2022.
Huko Ndjamena, maandamano dhidi ya serikali yalishika kasi tarehe 20 Oktoba 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi umefunguliwa kuhusu matukio ya Oktoba 20. Mwendesha mashtaka yuko katika gereza la Koro Toro, gereza lenye ulinzi mkali ambapo baadhi ya wafungwa wamehamishwa. Kwa kusubiri hitimisho la uchunguzi, serikali imetoa hoja zake, na imekusanya faili inayowasilisha maono yake ya kile kilichotokea.

Katika faili hili la takriban kurasa kumi, mamlaka inafafanua nukta kwa nukta maono yake ya kile kilichotokea. Oktoba 20 kulikuwa kulipangwa kuanzishwa kwa uasi. Upinzani ulitaka kuzusha ghasia kwa kuwashawishi wananchi, kuzusha mapigano makali hadi vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kupigwa marufuku kwa maandamano kwa kweli kulikusudiwa kugeuza mpango huu. Lakini asubuhi, vijana waliojihami kwa mapanga, visu, kombeo na bunduki walifanya mashambulizi, kwa mujibu wa Aziz Mahamat Saleh, msemaji wa serikali.

Ni lazima tuifanye nchi isidhibitike na upande wowote na kuigawanya Chad. Hilo ndilo lilikuwa lengo na kwa hivyo kwa njia zote, pamoja na njia hizi za uasi. Unaposhambulia makazi ya spika wa Bunge, kambi ya jeshi, kituo cha polisi, ni kweli ni maandamano ya amani. Lakini naamini kuwa mbali na faili hili, lililo muhimu ni lile litakalokuwa la kisheria litakaloundwa kupitia ushahidi halisi utakaowezesha kuweza kupata wale wote waliohusika.

Mpinzani Succès Masra alengwa na mamlaka

Mamlaka zimekusanya picha, taarifa, nyaraka rasmi za kuunga mkono toleo lao. Mwanasiasa wa upinzani Succès Masra ametajwa kuwa wa kwanza kuwajibika, pamoja na Chama Sans Frontières, Chama cha Atakhadoum na vuguvugu la Wakit Tama.

Kuhusu polisi, "walijilinda," inasema serikali. Hata hivyo serikali inatambua kwamba "wanakabiliwa na hali isiyotarajiwa na isiyo ya kawaida, hawakuweza kujizuia", "na kilichopaswa kutokea kilifanyika", inabainisha nakala hiyo.

Uchunguzi unaendelea ili kufafanua idadi ya waathiriwa na waliokamatwa. Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mateso inasema kuhusu watu 50 hadi 150 waliofariki, zaidi ya 150 hawajulikani waliko, karibu watu 1,400 walikamatwa, na hatimaye watu 600 hadi 1,100 kupelekwa katika gereza la Koro Toro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.